Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Thobias Makoba akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri za Mbeya, Songwe, na Iringa
Hii ni baada ya mazungumzo mafupi na Maafisa Habari hao ambayo yamejikita kwenye utendaji kazi baina yao na namna ya kuboresha vitengo vya mawasiliano katika maeneo yao ya kazi.
Kikao hicho kimefanyika mara baada ya kushiriki uzinduzi wa Kongamano la wadau na wananchi wa Nyanda za Juu Kusini, kuhusu ukusanyaji wa maoni ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Eden Highlands Hotel, Agosti 3, 2024 jijini Mbeya.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.