• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua ya Pepe |
Busokelo District Council
Busokelo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Takwimu
      • Fedha na Biashara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Usafishaji na Mazingira
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Ujenzi na Zima moto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Ufugaji Nyuki
    • Viwanda
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha Utawala na Mipango
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Elimu Afya na Maji
      • Kamati ya kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba ya vikao vya Madiwani
      • Ratiba ya kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti
    • Fomu za Maombi
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Vivutio vya Uwekezaji

Madini

Mawe ya Granit (matale) yanapatikana katika eneo la Kipangamansi lililopo Kijiji cha Kikuba. Inasemekana kwamba mawe haya yanapatikana kwatika nchi mbili tu duniani ikiwamo Tanzania. Mawe hayo bado hayajaanza kuchimbwa kiasi chakuwawezesha wawekezaji kujihusisha katika uchimbaji madini katika eneo hilo na kusaidia kuinua uchumi wa wakazi wa Hlmashauri na nchi kwa ujumla.

 

Kilimo na Ufugaji

Kilimo

Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo ina ukubwa wa eneo la hekta 96,914.0 (969.14 km2). Eneo lifaalo kwa kilimo ni hekta 49,389.67 na eneo linalolimwa kwa sasa ni hekta 43,569.76 sawa na asilimia 88.21 ya eneo linalofaa kwa Kilimo. Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo ina jumla ya kaya zinazojishughulisha na kilimo 24,133 zenye wastani wa wakulima 72,399. 

Kilimo cha umwagiliaji

Kuna jumla ya hekta 2695 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji, Hata hivyo fursa hiyo imetumika kwa kiwango cha asilimia 27 tu sawa na hekta 715.

Ufugaji

Ufugaji wa wanyama ni miongoni mwa shughuli muhimu mno za uchumi wa wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Halmashauri inakadiriwa kuwa na wanyama 313,610 ambapo 33,768 ni ng’ombe, 1,907 mbuzi na 991 kondoo. Wanyama wengine wanaofugwa ni nguruwe 12812, kuku wa kienyeji 258,827, kuku wa kisasa 2345, punda 75, Bata 659, Bata Mzinga 83, Kanga 127, Paka 713. Ufugaji umekuwa ukiendeshwa kiasili na kisasa ambapo ng’ombe wa kiasili ni 12556 na 21512 ni wa kisasa.

Uzalishaji na usindikaji maziwa

NA
KATA
UZALISHAJI/MWAKA (LITA)
1
Kandete
3,962,451
2
Luteba
4,705,137
3
Mpombo
2,301,638
4
Isange
6,858,175
5
Lwangwa
2,542,002
6
Kabula
1892,431
7
Lupata
1445,519
8
Itete
1321,713
9
Lufilyo
1143,025
10
Kisegese
963,382
11
Kambasegela
1286,529


28,422,002
  • Fursa za uzalishaji maua

Uzalishaji wa maua katika Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo ni moja ya shughuli za kiuchumi ambazo hazipewi nafasi na jamii kutokana na kukosa elimu juu ya zao hilo. Lakini kutokana na uwepo wa uwanja wa ndege wa kimataifa uliopo Songwe na hali nzuri ya hewa, Halmashauri imekuwa ikiwaalika wawekezaji kuendesha shughuli hiyo ili kutoa elimu kwa wenyeji wetu pia kuinua uchumi wetu kwa ujumla. Shughuli hii inaweza kufanywa katika eneo la uzalishaji lina ukubwa wa hekata 329. Kilimo cha mkataba kimekuwa kikihamasishwa kwa ajili ya kilimo cha maua katika Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo.

  • Fursa za uwekezaji katika usindikaji

Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo inafaa mno kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vya usindikaji wa mazao. Hilo linatokana na ukweli kuwa Halmashauri ina hali nzuri ya hewa kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya biashara (cocoa) nay ale ya chakula (mpunga). Kwa mfano uzalishaji wa cocoa kwa mwaka 2013/14 ulikuwa ni tani 8309.5 na mpunga tani 1773.9 lakini hakuna kiwanda chochote cha usindikaji wa mazao hayo ili ,uongeza thamani ya uzalishaji wa mazao hayo. Kwa hiyo uwekezaji katika viwanda vya usindikaji ni jambo muhimu mno kwa ajili ya maendeleo ya maeneo ya Vijijini ili kuongez thamani ya malighafi za mazao ya kilimo na kuhamasisha soko la mazao ya shanbani.

 

  • Uzalishaji Samaki

Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo ina utajiri mkubwa wa maziwa ambayo yanaweza kutumika kwa ajili ya shughuli za uvuvi kwa ajili ya viwanda vya samaki. Maziwa hayo yana uwezo wa kuzalisha samaki kwa ajili ya matumizi na faida kwa ajili ya iashara. Miongoni mwa maziwa hayo ni Kyungululu, Kingili, Ilamba, Ikapu, Itamba na Itende. Uwekezaji unaoweza kufanywa katika maziwa hayo ni ufugaji samaki ambapo aina tofauti za samaki zinaweza kufugwa katika maziwa hayo.

  • Ufugaji Nyuki

Ufugaji wa nyuki katika Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo ni shughulinya kiuchumi inayoendeshwa na jamii, hata hivyo Halmashauri haina wafugaji wengi wa nyuki wanaofuga kwa ajili ya biashara. Lakini kwa sasa wananchi wamekuwa wakijiingiza kwa wingi katika ufugaji wa nyuki katika Vijiji vingi na wameunda makundi ya ufugaji nyuki kwa ajili ya kuzalisha asali na nta katika kiwango cha juu. Maeneo yote katika Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo yana mazingira rafiki kwa ajili ya shughuli za ufugaji nyuki. Shughuli hizo zinafanywa katika maeneo yenye maji na idadai kubwa ya Hifadhi ya misitu kama hifadhi yam situ wa Kyejo, hifadhi ya msitu wa mlima Livingstone, Ngeleka, Ivolelo, Katebhele na mingineyo

  • Fursa za uwekezaji katika Utalii

Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo ina vivutio vya asili vya uitalii na yapo maeneo ya kutosha yenye vivutio kwa ajili ya shughuli za utalii.

  • Maporomoko ya maji

Halmashauri imebarikiwa kuwa na maporomoko ya maji yaliyopo katika mito mbalimbali mfano maporomoko ya Ntete yanayopeleka maji katika mkondo Ntete, maporomoko ya Busango yanayotiririsha maji katika mkondo wa Busango, Mwasambi, Mbande, Kalebwa na kwamba maporomoko yote hayo ya maji yanapeleka maji yake katika mto Lufilyo kabla ya kufika ziwa Nyasa huku maporomoko mengine ya maji yakipeleka maji yao katika ziwa Mbaka yakiwamo maporomoko ya Itupi na Mambwe I&II. Maporomoko hayo ya maji yanaweza kutumika kama vivutio vya utalii lakini pia chanzo cha kuzalisha umeme wa maji (hydropower). Pia yanaweza kutumika kwa ajili ya kutengeneza maji ya chupa.

  • Daraja la Mungu la Mambwe

Halmashauri imebarikiwa kuwa na daraja la asili lililopo katika mto Mambwe uliopo Kijiji cha Nsoso. Maji yanayoingia lililopo daraja hilo yanafanya hivyo kwa kasi ya aina yake, lakini yanayotoka kasi yake ni ndogo. Inaonesha kwamba kuna nguvu ya asili chini ya daraja hilo inayopunguza kasi ya maji.

Daraja hilo lina mvuto wa aina yake katika shughuli za mlima Kyejo, huu ni mlima wa volcano na unapoupanda utakutana na vivutio lukuki kama udongo wa volcano, majani ya volcano, matundu ya volcano, nyasi fupi na maua. Pia kunapatikana majani ya kipekee juu ya mlima huo. Mlima una vilele vitatu, viwili vya kwanza vikiwa vimekaribiana na kingine kirefu Zaidi kikiwa pande mwingine wa mlima.

  • Chemchem ya Kilambo

Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo imejaliwa kuwa na chemchem inayotoa maji ya moto inayofahamika kama Kilambo. Chechem hiyo ya kustajaabisha, inapatikana katika Kata za Kambasegela na Lupata. Chemchem hiyo imekuwa kivutio kikubwa cha watalii, pia imekuwa chanzo chamaji moto ambayo yamekuwa yakitumika kwa shughuli za kilimo na ufugaji. Inashauriwa kuwa eneo hili linatakiwa kuhifadhiwa kwani ni kivutio kikubwa cha utalii kutokana na chemchem yake ya maji ya moto.

Ufuatao ni mwonekano wa chemchem ya Kilambo:

  1. Ni ya kudumu, maji yake hayaomngezeki wala kupungua
  2. Kutokana na maji yake kuwamoto sana unaweza kuchemsha yai au viazi mbatata
  3. Maji yake ni masafi na yanavutia kuyatazama, Pembezoni mwa chemchem hiyo, kuna ardhi yenye rutuba lakini hakuna shughuli yeyote ya kiuchumi inayoendelea, hii inatokana na ukweli kwamba bado hakuna uelewa juu ya umuhimu wa kuwekeza katika eneo hilo.
  4. Chemchem za Kilambo zinapeleka maji katika mto hivyo ni chanzo cha mto katika eneo hilo.

 

  • Mapango

Busokelo ina mapango mawili makubwa yanayopatikana pembezoni mwa mto Lufilyo ambayo ni Kipapa na pango la Makwitwa linalopatikana katika misitu ya Ivolelo katika Kijiji cha Kipyola. Pango la Kipapa limetokana na mawe na ni kubwa kiasi ambacho watu saba au nane wanaweza kuingia pamoja. Pango hilo lina mwonekano mzuri wa kiutalii na unapolichungulia unaweza kuona maporomoko ya maji.

  • Pango la Makwitwa

Pango la Makwitwa linapatikana katika msitu wa Ivolelo na mdomo wa pango hilo ni duara kati ya watu watani hadi sita wanaweza kuingia wakati mmoja

  • Maziwa

Kuna mabonde kadhaa yanayopatikana katika Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo ambayo ni Kyungulu, Kingili, Ilamba, Ikapu, Itamba, Itende, Kyambangungulu, Lusiba na Kyejo. Kutokana na mandhari yake, maziwa yanafaa Zaidi kwa kuweka mapumziko, kujenga hoteli za kitalii na shughuli nyingine za kitalii. Lakini shughuli za utunzaji mazingira zinatakiwa kupewa kipaumbele ili kuendeleza hali yake ya kuvutia

  • Ziwa Kyungulu

Ndilo ziwa lenye kina kirefu kuliko yote Busokelo, lina mandhari nzuri kwa shughuli za utalii, kujipumzisha, kuogelea na kuweka hoteli za kitalii, ziwa hili linapatikana katika Kata ya Itete.

  • Ziwa Kingili

Ni kubwa na limezungukwa na miti ya asili ambayo inatoa hewa safi na ya asili lina eneo zuri linalofaa kwa ujenzi wa hoteli na kuendesha shughuli za kitalii. Pia ziwa hilo lina mamba ambao ni kivutio kikubwa cha watalii, ziwa hili linapatikana katika Kata ya Kisegese.

  • Ziwa Ilamba

Ziwa hili linapatikana katika Kata ya Kambasegela. ni kubwa lenye kina kirefu na pia lina mamba, limezungukwa na miti ya aina tofauti ambayo imekuwa ikichangia kubadil;ika kwa hali ya hewa katika maeneo yanayozunguka ziwa hilo.

  • Ziwa Ikapu

Ziwa hili linapatikana katika Kata ya Kambasegela. ni kubwa, ni kubwa lina mamba na bata mzinga, ziwa hili linavutia sana watalii hasa kutokana na upepo wake mkali.

  • Ziwa Itende

Moja kati ya maajabu makubwa ya ziwa Itende, linapatikana juu ya mlima. Juu yake unaweza kuona maziwa matatu ambayo ni Ikapu, Kisiba, na Nyasa. Ni eneo zuri kwa shughuli za utalii, kabla ya kufika ziwa Itende unatakiwa kuvuka daraja la Mungu. Pia unakutana na daraja dogo liitwalo Kindandali na ni chanzo cha ziwa Itende. Ziwa hili linapatinana katika Kata ya Lupata.

Ziwa Kyamba Ngungulu

Ziwa hili linaptikana katika mlima Ngungulu na linahitaji uangalizi ili kulitunza kwani limechakaa mno, ziwa Kyamba Ngungulu linafaa Zaidi kwa ufugaji wa samaki kutokana na msitu mkubwa uliopo, hata ufugaji wa nyuki unafaa katika eneo hili. Ziwa hili liko katika Kata ya Kambasegela.

  • Ziwa Lusiba

Linapatikana katika Kata ya Mpombo na ni kubwa licha ya shughuli za binadamu kuonekana kuliharibu, Halmashauri inatakiwa kuwekeza nguvu katika kurejesha hadhi ya ziwa hili. Mbali na utalii, shughuli za uvuvi pia zinaweza kufanywa katika eneo hili.

  • Ziwa Kyejo

Ziwa hili linapatika juu ya mlima Kyejo, lakini pia limekuwa likiharibiwa na shaghuli za binadamu. Kutoakana na hilo umeonekana kupungua. Ziwa hili ni kivutio kikubwa cha watalii.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA USAILI WA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA. December 09, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA AJIRA YA MKATABA October 20, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI MOJA YA AJIRA April 11, 2023
  • TANGAZO LA UKODISHAJI MAGHALA YA KUHIFADHIA KOKOA June 05, 2024
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MHE. HOMERA AHIMIZA USHIRIKIANO WA WANANCHI NA SERIKALI UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO.

    June 11, 2025
  • KIDELI SASA BASI, CHANJO YA KUKU YA YAZINDULIWA RASMI BUSOKELO.

    June 09, 2025
  • MAFANIKIO SEKTA YA KILIMO HALMASHAURI YA BUSOKELO MWAKA 2024/2025.

    June 06, 2025
  • KAMPUNI YA UJENZI WA BARABARA YA CHINA ROADS AND BRIDGE CO-OPERATION YASAINI MKATABA WA KUWA MPANGAJI KATIKA MAKAMBI YA MBAMBO.

    May 29, 2025
  • Angalia zote

Video

Mkurugenzi atoa hamasa ya chakula kwa watoto mashuleni
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Watumishi Portal
  • Hati ya Mshahara
  • Orodha ya Madiwani
  • Maktaba ya Picha

Viunganishi Linganifu

  • Utumishi wa Umma
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Tovuti ya Rais
  • Tovuti ya Mkoa wa Mbeya
  • Sekretarieti ya Ajira

Kipimo cha Wateja duniani

world map hits counter

Wateja waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Lwangwa, Tukuyu

    Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu

    Simu: +255 737 205 318

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.