MHE. HOMERA AHIMIZA USHIRIKIANO WA WANANCHI NA SERIKALI UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera amefanya ziara rasmi katika Halmashauri ya Busokelo lengo ikiwa ni kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo 11Juni, 2025.
Katika ziara hiyo,Dkt.Homera ametembelea mradi wa barabara ya Lwangwa-kyejo unaogharimu kiasi cha shilingi billion 6, mradi huo umefikia asilimia 97, ameagiza wataalamu na mkandarasi kuhakikisha kuwa kufikia 10 julai 2025 mradi huo unakamilika.
Sambamba na hilo, Dkt. Homera amepata nafasi ya kutembelea mradi wa vioski vitano(5) vya maji unaotekelezwa na serikali katika kata ya Ntaba unaogharimu kiasi cha shilingi million 300 mradi huo umefikia asilimia 100 za ukamilishaji. Mhe. Dkt.Homera amegiza kuwa vioski hivyo visimamiwe vizuri na viendeshwe kwa ufasini ili wananchi wapate maji safi na salama.
Mhe.Dkt Juma Homera ameongoza mkutano wa hadhara katika eneo la ofisi za kijiji cha Mbambo,katika mkutano huo ametoa taarifa kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kusikiliza changamoto zinazowakumba wananchi,amewaahidi wananchi kuwa serikali ya Awamu ya sita ikiongozwa na Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan inaendelea kuboresha huduma za kijamii ikiwemo maji,umeme na barabara.
Aidha,Dkt.Homera amewataka wananchi kushirikiana kikamilifu na wataalamu pamoja na viongozi ili kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inakamilika kwa ubora na wakati unaotakiwa.Amesema kuwa serikali inaendelea kusimamia na kufuatilia kwa ukaribu miradi ili kuhakikisha Wananchi wanapata maendeleo ya haraka na yenye tija.
Ziara ya Mkuu wa Mkoa Mhe.Dkt. Juma Zuberi Homera katika Halmashauri yaWilaya ya Busokelo inaashiria nia ya Serikali kuendelea kuleta mabadiliko chanya na kuboresha maisha ya wananchi wa Busokelo kwa ujumla.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.