• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Busokelo District Council
Busokelo District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Busokelo District Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Adminstration
    • Organization Structure
    • Departments
      • Adminstration and Human Resource
      • Planning and Statistics
      • Finance and Trade
      • Primary Education
      • Secondary Education
      • Health
      • Water
      • Sanitation and Environment
      • Agriculture, Irrigation and Cooperatives
      • Livestock and Fisheries
      • Development and Social Walfare
      • Land and Natural Resouces
      • Construction, Fire and Works
    • Units
      • Internal Audit
      • Bee Keeping
      • Election
      • Legal
      • Ict
      • Procurement and Supplies
  • Investment Oppotunities
    • Tourism
    • Agricultural
    • Livestock
    • Fishing
    • Bee Keeping
    • Industries
  • Our Services
    • Health
    • Education
    • Water
    • Agriculture
    • Livestock
    • Fishing
  • Councilors
    • Councilors list
    • Standing Committee
      • Finance Planning and Adminstration
      • Economy Works and Environment
      • Education Health and Water
      • CMAC
      • Ethics committee
    • Schedules
      • Councilors schedule meetings
      • Chairperson schedule
  • Projects
    • Planned projects
    • On going projects
    • Completed projects
  • Publications
    • Acts
    • Customer service contrct
    • Strategic plan
    • Reports
    • Application Forms
    • Guidelines
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery

SHIRIKIANENI NA WATENDAJI WA VIJIJI KUWAHUDUMIA WANANCHI.

Posted on: December 11th, 2024

SHIRIKIANENI NA WATENDAJI WA VIJIJI KUWAHUDUMIA WANANCHI.


Viongozi wa Serikali za Vijiji wametakiwa kufunya kazi kwa weledi, uzalendo na  moyo wa kujituma kwa kushirikiana na Watendaji wa vijiji ili kuwatumikia Wananchi kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa leo 11/12/2024 na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo Mhe.Anyosisye Njobelo wakatika akifungua Mafunzo ya Uongozi na Utumishi kwa Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na Wajumbe wa Halmashauri za vijiji katika Kata za Mpombo, Kandete, Isange na Luteba.

Zaidi ya Viongozi 400 wa Serikali za Vijiji wakiwemo Wenyeviti wa Vijiji,Wenyeviti wa Vitongoji na Wajumbe wa Halmashaurui za vijiji kutoka ukanda wa Mwakaleli wamepatiwa mafunzo ya Uongozi katika bwalo la Mwakaleli Sekondari ili kuwajengea uwezo wa namna ya kuwatumikia Wananchi katika nafasi mbalimbali za uongozi walizochaguliwa  katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.

‘’Baada ya kuchaguliwa na Wananchi wenu, mlikula kiapo cha utii, Mafunzo haya muyatumie vizuri ili mkawatumikie Wananchi katika vijiji venu, kuweni wazalendo, mkashirikiane na Watendaji wa vijiji  kutatua kero zote katika maeneo yenu kwa haki, usawa na kujituma ili muwaletee maendeleo Wananchi waliyo wachagua” alisema Mhe.Njobelo.

Kwa Upande wake Afisa Utumishi Halmshauri ya Wilaya ya Busokelo Bw.Fredrick Kweka aliwasilisha mada kuhusu Majumuku ya Wenyeviti wa vijiji, Wenyeviti wa vitongoji na Wajumbe wa Halmashauri za vijiji  pamoja na majukumu ya Mtendaji wa kijiji na wajibu wa Serikali za vijiji kwa Wananchi ili kuongeza uelewa  katika utekelezaji majukumu kwa viongozi hao.

Katika Hatua nyingine Afisa Mapato Halmsahauri ya Busokelo Bi.Abella Ndamugoba aliwajengea zaidi uwezo Viongozi wa Serikali za vijiji kuhusu madhara ya utoroshaji wa mapato na umuhimu wa kusimamia ukusanyaji wa maopato katika vijiji huku akiwataka kutowafumbia macho wale wote wanao shiriki katika utoroshaji mapato kwenye vijiji kwani wanadhoofisha maendeleo ya kijiji husika.

Aidha Bw.Elia Msukwa Afisa Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo aliwaeleza Viongozi hao namna ambavyo migorororo ya ardhi inavyokwamisha shughuli za maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na kijiji kwa ujmla huku akiwataka kutokuwa chanzo cha migogoro ya ardhi na badala yake waishauri jamii kufikia mwafaka mzuri katika utatuzi wa migogoro ya ardhi kwa kuzingatia sheria kanuni na miongozo iliyowekwa.

Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, Idara ya Utawala na Rasilimali Watu imeratibu mafunzo ya uongozi na utumishi kwa viongozi wote Serikali za Mitaa waliyongia madarakani  mwaka 2024 katika kata zote 13 za Busokelo ili kuwajengea uwezo wa kutwekeleza majukumu yao.

Tayari Viongozi wa vijiji kutoka kataza Isange, Kandete, Luteba,Mpata, Kabula, Lwangwa na Lupata wameshapatiwa mafunzo ya Uongozi , zoezi la utoaji mafunzo hayo linaendelea katika ukanda wa Lufilyo.


Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA USAILI WA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA. December 09, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA AJIRA YA MKATABA October 20, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI MOJA YA AJIRA April 11, 2023
  • TANGAZO LA UKODISHAJI MAGHALA YA KUHIFADHIA KOKOA June 05, 2024
  • View All

Latest News

  • MHE. HOMERA AHIMIZA USHIRIKIANO WA WANANCHI NA SERIKALI UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO.

    June 11, 2025
  • KIDELI SASA BASI, CHANJO YA KUKU YA YAZINDULIWA RASMI BUSOKELO.

    June 09, 2025
  • MAFANIKIO SEKTA YA KILIMO HALMASHAURI YA BUSOKELO MWAKA 2024/2025.

    June 06, 2025
  • KAMPUNI YA UJENZI WA BARABARA YA CHINA ROADS AND BRIDGE CO-OPERATION YASAINI MKATABA WA KUWA MPANGAJI KATIKA MAKAMBI YA MBAMBO.

    May 29, 2025
  • View All

Video

Mkurugenzi atoa hamasa ya chakula kwa watoto mashuleni
More Videos

Quick Links

  • Watumishi Portal
  • Salary slip
  • Councilors list
  • Gallery

Related Links

  • President's Office, Public Service Management
  • TAMISEMI
  • e-Government Agency
  • President's Officia Website
  • Mbeya Regional Website
  • Public Service Recruitment Secretariet

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Lwangwa, Tukuyu

    Postal Address: S. L. P. 2, Tukuyu

    Telephone: +255 737 205 318

    Mobile:

    Email: ded@busokelodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2019 Busokelo DC . All rights reserved.