Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo ni miongoni mwa Halmashauri mpya za Wilaya zilizoanzishwa nchini Tanzania na ikiwa imegawanywa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe mwaka 2012 baada ya mlolongo wa mageuzi nahitaji la kutoa huduma bora na za kutoshwa kwa jamii.
Historia ya Kijiografia
Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo inapatikana kati ya latitude 80 30’mashariki 90 30’kusini mwa ikweta na longitudo 33’ na 34’ mashariki mwa greenwich meridian.Halmashauri inapakana na Wilaya ya Kyela kwa upande wa kusini, Halmashauri yaWilaya ya Rungwe kwa upande wa magharibi, Wilaya ya Makete kwa upande wamashariki na Wilaya ya Mbeya iliyopo upande wa kaskazini. Makao makuu yaHalmashauri ya Wilaya ya Busokelo yapo Mji wa Lwangwa ambao upo kilomita 47kutoka Tukuyu mjini.
Eneo laardhi
Halmashauri ina jumla ya eneo la kilomita za mraba 969.14 ambapoasilimia 85 ya eneo hilo linatumika kwa ajili ya kilimo wakati ardhi iliyobakiasilimia 15 zikiwa zimetawaliwa na misitu, milima na maeneo ya makazi
Hali yahewa
Hali ya hewa ya Wilaya hii inatokana na urefu wake kutoka usawawa bahari, Wilayah ii ni ya milima ambapo kuna mlima Rungwe na Livingstoneambayo ipo mita 770 hadi 2,265 kutoka usawa wa bahari. Wastani wa mvua nimilimita 900 kwenye maeneo ya tambarare hadi milimita 2,700 kwa maeneo yenyemiinuko. Kwa kawaida joto linakadiliwa kuwa nyuzi joto 18-25 kwa kipindi chotecha mwaka.
ORODHA YA WAKURUGENZI WATENDAJI WALIOFANYA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA BUSOKELO
NAMBA
|
JINA KAMILI
|
MWAKA
|
1
|
Imelda L. Ishuza
|
2012 - 2014
|
2
|
Said A. Mderu
|
2014 - 2015
|
3
|
Dr. Leonard M. Masale
|
2015 - 2016
|
4
|
Eston P. Ngilangwa
|
2016 -
|
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.