Utangulizi
Idara ya Ujenzi ni miongoni mwa idara na vitengo vinavyoiunda Halmashauri ya Wilaya Busokelo.
Ilianza kujitegemea rasmi mwaka 2013 baada ya kuanzishwa Halmashauri ya Wilaya Busokelo, kwani kabla ya hapo ilikuwa chini ya Halmashauri ya Wilaya Rungwe.
Utekelezaji
Idara ina vitengo vifutavyo:
Kitengo hiki kazi yake kuu ni kuratibu kazi za matengenezo ya barabara za Halmashauri ya Wilaya. Ikumbukwe kuwa, Barabara zilizopokatika Wilaya zimegawanywa katika makundi yafuatayo:
Hizi ni barabara zinazotunzwa na TANROADS. Barabara hizi zina sifa zifuatazo: zinaunganisha makao makuu ya Wilaya na Mkoa, Makao makuu ya Wilaya na Wilaya, au zinaunganisha Wilaya na barabara kuu n.k
Katika kundi hili kuna barabara zenye kuwa na sifa zifuatazo: barabara zinazounganisha makao makuu ya kata na Wilaya, kata na kata, Tarafa na kata, barabaraza mijini . Halmashauri ya Wilaya inahudumia mtandao wa barabara zenye urefu wa 510Km .
Hizi ni barabara zinazounganisha kijiji na kijiji,kitongoji na kijiji.
Barabara zilizo chini ya jamii zina urefu wa 430Km .
Jukumu kuu la idara ya ujenzi ni kuhakikisha barabara zinazohudumiwa na Halmashauri na Jamii zinaendelea kutengenezwa na kupitika aidha kwa kutoa ushauri katika jamii husika( Community roads) namna bora yakuzifanyia matengenezo barabara hizo.
Halmashauri ina barabara za mijini(urban roads ) katika miji ya Lwangwa makao makuu ya wilaya na Kandete. Kwa kuwa miji hii inakuwa kwa kasi, ni jukumu la Halmashauri ya Wilaya kupitia idara ya Ujenzi kuhakikisha miundombinu ya barabara inatengenezwa namajengo yanafuata taratibuza mipango miji.
Katika mwaka wa fedha 2015/2016 Halmashauri iliendelea kufungua barabara ili kuboresha huduma za jamii.
Pia Serikali ya Uingereza kupitia shirika lake la maendeleo (DFID) imeweza kufadhili miradi ya Ujenzi wa barabara na madaraja ili kuimarisha sekta ya usafiri vijijini.
Kazi kubwa ya kitengo hiki ni kusimamia na kuratibu kazi za Majengo ya serikali na jamii. Majengo ya serikali yanayosimamiwa na kitengo hiki ni Majengo ya kutolea huduma za afya, Kilimo, Elimu, Utawala. N.k. Hata hivyo, ushauri kwa wananchi wanaopenda kujenga nyumba za bei nafuu na imara (zenye Kufuata taratibu za Kihandisi) umekuwa ukitolewa ili kuwa na majengo yenye tija. Sambamba na hilo kwa kushirikiana na idara ya ardhi tumeanzisha utaratibu wa kupitia michoro kwa kila mwananchi anayetaka kujenga nyumba yake katika mji wa Lwangwa na kandete ili kuhakikisha Ujenzi unakuwa wenye tija na unaofuata taratibu za mipango miji.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.