Fursa za uwekezaji katika usindikaji
Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo inafaa mno kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vya usindikaji wa mazao. Hilo linatokana na ukweli kuwa Halmashauri ina hali nzuri ya hewa kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya biashara (cocoa) nay ale ya chakula (mpunga). Kwa mfano uzalishaji wa cocoa kwa mwaka 2013/14 ulikuwa ni tani 8309.5 na mpunga tani 1773.9 lakini hakuna kiwanda chochote cha usindikaji wa mazao hayo ili ,uongeza thamani ya uzalishaji wa mazao hayo. Kwa hiyo uwekezaji katika viwanda vya usindikaji ni jambo muhimu mno kwa ajili ya maendeleo ya maeneo ya Vijijini ili kuongez thamani ya malighafi za mazao ya kilimo na kuhamasisha soko la mazao ya shambani.
Usindikaji maziwa
Ufugaji wa wanyama ni miongoni mwa shughuli muhimu mno za uchumi wa wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Halmashauri inakadiriwa kuwa na wanyama 313,610 ambapo 33,768 ni ng’ombe, 1,907 mbuzi na 991 kondoo. Wanyama wengine wanaofugwa ni nguruwe 12812, kuku wa kienyeji 258,827, kuku wa kisasa 2345, punda 75, Bata 659, Bata Mzinga 83, Kanga 127, Paka 713. Ufugaji umekuwa ukiendeshwa kiasili na kisasa ambapo ng’ombe wa kiasili ni 12556 na 21512 ni wa kisasa.
Uzalishaji na usindikaji maziwa
NA
|
KATA
|
UZALISHAJI/MWAKA (LITA)
|
1
|
Kandete
|
3,962,451
|
2
|
Luteba
|
4,705,137
|
3
|
Mpombo
|
2,301,638
|
4
|
Isange
|
6,858,175
|
5
|
Lwangwa
|
2,542,002
|
6
|
Kabula
|
1892,431
|
7
|
Lupata
|
1445,519
|
8
|
Itete
|
1321,713
|
9
|
Lufilyo
|
1143,025
|
10
|
Kisegese
|
963,382
|
11
|
Kambasegela
|
1286,529
|
|
|
28,422,002
|
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.