RC MALISA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA BUSOKELO.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Beno Malisa amefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mhe. Malisa akiongozana za Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa amepitia na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa mradi ujenzi wa vioski vitano vya majini pamoja uchimbaji wa visima wenye thamani ya shilingi milioni 300 chini ya RUWASA kwa lengo kufikisha huduma bora za maji safi na salama kwa Wakazi wa Kata ya Ntaba.
Katika Ziara hiyo Mhe.Malisa ameagiza wataalamu wanaosimamia utekelezaji wa miradi hiyo kuhakikisha ina kamilika kwa wakati na kuendana na viwango vinavyokusudiwa.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bw.Rodrick Mpogolo amesisitiza kuhusu utunzaji wa nyaraka zote za miradi kwa ajili rejea mbalimbali ikiwemo masuala ya ukaguzi.
Miradi mingine iliyokaguliwa ni pamoja na ujenzi wa ofisi ya kijiji cha Kandete ambapo kiasi cha shilingi milioni 65.8 kimetengwa kupitia mapato ya ndani ya Halamshauri ili kutekeleza ujenzi huo.
Mradi wa ukamilishaji wa zahanati ya kikuba unaogharimu kiasi cha shilingi milioni 142.7, ujenzi wa Barabara ya Lwangwa-Kyejo yenye kiwango cha lami wenye thamani ya shilingi bilioni 6.1 pamoja ujenzi wa bweni la Wanafunzi katika shule ya Sekondari Lwangwa wenye thamani ya shilingi milioni 189.7
Aidha Mhe. Malisa amekagua kikundi vijana wa bodaboda WASTARABU Kata ya Lwangwa amabao ni Wanufaika wa mkopo wa shilingi milioni 16 kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri, Kamati ya Usalama Mkoa wa Mbeya imewataka vijana hao kuendesha shughuli za kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.