HUDUMA ZA AFYA
Utoaji waHuduma za Afya
Halmashauri ina Hospitali 1, ambayo ni ya ubia kati ya Serikalina na Madhehebu la Dini (CDH), kituo 1 cha Afya na zahanati 18 kati yake 12 niza Serikali na 6 ni za Madhehebu ya Dini .Wastani wa umbali wa Zahanatitoka kwa mtu aliye mbali na huduma hiyo ni kilomita 6.7. Kitaifa, wastani kwamtu aliye mbali na huduma hiyo ni k.m. 10. Vituo vyote vinasimamiwa naKamati za Uendeshaji chini ya Bodi ya Huduma ya Afya ya Halmashauri.
MapambanoDhidi ya VVU/UKIMWI
Halmashauri ya Busokelo inakabiliwa na janga la UKIMWI kamailivyo sehemu zingine na kusababisha ongezeko la watoto yatima. Kati ya mwaka2012 hadi Juni, 2014 jumla ya watu 5420 wamepima afya zao kwa hiari . HadiJuni, 2014 watu wanaopata dawa ya kurefusha maisha ni 2636. Hali ya maambukiziVVU/UKIMWI ni asilimia 9. Jitihada za kuwaelimisha wananchi kujikinga namaambukizi mapya ya UKIMWI zinaendelea.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.