JUMLA YA MIRADI YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 171. YAKAGULIWA NA KAMATI YA UKAGUZI.
Kamati ya Ukaguzi wa Miradi Halmashauri ya Busokelo leo 14/07/2025 imekagua na kupongeza katua za utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi milioni 171.
Miongoni miradi iliyokaguliwa ni pamoja na ujenzi wa Bweni la Wanafunzi katika shule ya Sekondari ya Wavulana Busokelo Kata ya Isange unaojengwa kupitia milioni 80 za mapato ya shule , hadi sasa mradi huo upo katika hatua ya linta.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi Halmashauri ya Busokelo Mwl.Wilbert Bendera alipongeza hatua za Ujenzi wa mradi huo huku akisisitiza kukamilika kwa mradi huo katika muda uliyopangwa ili Wanafunzi waanze kutumia Bweni hilo.
Aidha katika hatua nyingine Kamati ilikagua ujenzi wa nyumba ya Mtumishi katika shule ya msingi Ipyela Kata ya Luteba wenye thamani ya shilingi milioni 51 kupitia mradi wa GPE-PSP, ujenzi upo katika hatua ya kupaua .Kamati iliwapongeza Wataalamu na Wananchi wanaosimamia ujenzi huo.
Katika hatua nyingine Kamati ilifika katika mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji Kata ya Kandete, ambapo Halmashauri imetenga kiasi cha Shilingi milioni 40 kupitia mapato ya ndani ili kutekeleza ujenzi huo, na mpaka sasa ujenzi upo katika hatua ya msingi na tayari mafundi wamekwisha mwaga jamvi katika msingi huo.
Katika kuhitimisha ziara ya ukaguzi Mwenyekiti wa Kamati Mwl.Bendera pamoja na wajumbe walipongeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwezesha utekelezaji miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Busokelo, na kuwahimiza Wananchi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kushiriki kimalilifu katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.