FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA UTALII
Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo ina vivutio vya asili vya uitalii na yapo maeneo ya kutosha yenye vivutio kwa ajili ya shughuli za utalii.
1.0 Maporomoko ya maji
Halmashauri imebarikiwa kuwa na maporomoko ya maji yaliyopo katika mito mbalimbali mfano maporomoko ya Ntete yanayopeleka maji katika mkondo Ntete, maporomoko ya Busango yanayotiririsha maji katika mkondo wa Busango, Mwasambi, Mbande, Kalebwa na kwamba maporomoko yote hayo ya maji yanapeleka maji yake katika mto Lufilyo kabla ya kufika ziwa Nyasa huku maporomoko mengine ya maji yakipeleka maji yao katika ziwa Mbaka yakiwamo maporomoko ya Itupi na Mambwe I&II. Maporomoko hayo ya maji yanaweza kutumika kama vivutio vya utalii lakini pia chanzo cha kuzalisha umeme wa maji (hydropower). Pia yanaweza kutumika kwa ajili ya kutengeneza maji ya chupa.
2.0 Daraja la Mungu la Mambwe
Halmashauri imebarikiwa kuwa na daraja la asili lililopo katika mto Mambwe uliopo Kijiji cha Nsoso. Maji yanayoingia lililopo daraja hilo yanafanya hivyo kwa kasi ya aina yake, lakini yanayotoka kasi yake ni ndogo. Inaonesha kwamba kuna nguvu ya asili chini ya daraja hilo inayopunguza kasi ya maji.
Daraja hilo lina mvuto wa aina yake katika shughuli za mlima Kyejo, huu ni mlima wa volcano na unapoupanda utakutana na vivutio lukuki kama udongo wa volcano, majani ya volcano, matundu ya volcano, nyasi fupi na maua. Pia kunapatikana majani ya kipekee juu ya mlima huo. Mlima una vilele vitatu, viwili vya kwanza vikiwa vimekaribiana na kingine kirefu Zaidi kikiwa pande mwingine wa mlima.
3.0 Chemchem ya Kilambo
Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo imejaliwa kuwa na chemchem inayotoa maji ya moto inayofahamika kama Kilambo. Chechem hiyo ya kustajaabisha, inapatikana katika Kata za Kambasegela na Lupata. Chemchem hiyo imekuwa kivutio kikubwa cha watalii, pia imekuwa chanzo chamaji moto ambayo yamekuwa yakitumika kwa shughuli za kilimo na ufugaji. Inashauriwa kuwa eneo hili linatakiwa kuhifadhiwa kwani ni kivutio kikubwa cha utalii kutokana na chemchem yake ya maji ya moto.
Ufuatao ni mwonekano wa chemchem ya Kilambo:
4.0 Mapango
Busokelo ina mapango mawili makubwa yanayopatikana pembezoni mwa mto Lufilyo ambayo ni Kipapa na pango la Makwitwa linalopatikana katika misitu ya Ivolelo katika Kijiji cha Kipyola. Pango la Kipapa limetokana na mawe na ni kubwa kiasi ambacho watu saba au nane wanaweza kuingia pamoja. Pango hilo lina mwonekano mzuri wa kiutalii na unapolichungulia unaweza kuona maporomoko ya maji.
(a) Pango la Kipapa
(b) Pango la Makwitwa
Pango la Makwitwa linapatikana katika msitu wa Ivolelo na mdomo wa pango hilo ni duara kati ya watu watani hadi sita wanaweza kuingia wakati mmoja
5.0 Mlima Kyejo
Huu ni mlima uliotokana na Volkano, ukipanda juu ya mlima huu utaona vitu vingi vya kuvutia kama vile mashimo makubwa ya volkano, uoto wa nyasi fupi za kupendeza sana pamoja na maua. Uoto huu wa nyasi unapatikana juu ya kilele cha mlima. Mlima una sifa ya kuwa na vilele vitatu, ambapo vilele viwili vinakaribiana sana wakati kilele cha tatu kipo upande wa pili wa vilele hivyo juu kabisa ya mlima.
6.0 Maziwa ya asili
Kuna mabonde kadhaa yanayopatikana katika Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo ambayo ni Kyungulu, Kingili, Ilamba, Ikapu, Itamba, Itende, Kyambangungulu, Lusiba na Kyejo. Kutokana na mandhari yake, maziwa yanafaa Zaidi kwa kuweka mapumziko, kujenga hoteli za kitalii na shughuli nyingine za kitalii. Lakini shughuli za utunzaji mazingira zinatakiwa kupewa kipaumbele ili kuendeleza hali yake ya kuvutia.
6.1 Ziwa Kyungulu
Ndilo ziwa lenye kina kirefu kuliko yote Busokelo, lina mandhari nzuri kwa shughuli za utalii, kujipumzisha, kuogelea na kuweka hoteli za kitalii, ziwa hili linapatikana katika Kata ya Itete.
6.2 Ziwa Kingili
Ni kubwa na limezungukwa na miti ya asili ambayo inatoa hewa safi na ya asili lina eneo zuri linalofaa kwa ujenzi wa hoteli na kuendesha shughuli za kitalii. Pia ziwa hilo lina mamba ambao ni kivutio kikubwa cha watalii, ziwa hili linapatikana katika Kata ya Kisegese.
6.3 Ziwa Ilamba
Ziwa hili linapatikana katika Kata ya Kambasegela. ni kubwa lenye kina kirefu na pia lina mamba, limezungukwa na miti ya aina tofauti ambayo imekuwa ikichangia kubadil;ika kwa hali ya hewa katika maeneo yanayozunguka ziwa hilo.
6.4 Ziwa Ikapu
Ziwa hili linapatikana katika Kata ya Kambasegela. ni kubwa, ni kubwa lina mamba na bata mzinga, ziwa hili linavutia sana watalii hasa kutokana na upepo wake mkali.
6.5 Ziwa Itende
Moja kati ya maajabu makubwa ya ziwa Itende, linapatikana juu ya mlima. Juu yake unaweza kuona maziwa matatu ambayo ni Ikapu, Kisiba, na Nyasa. Ni eneo zuri kwa shughuli za utalii, kabla ya kufika ziwa Itende unatakiwa kuvuka daraja la Mungu. Pia unakutana na daraja dogo liitwalo Kindandali na ni chanzo cha ziwa Itende. Ziwa hili linapatinana katika Kata ya Lupata.
6.7 Ziwa Kyamba Ngungulu
Ziwa hili linaptikana katika mlima Ngungulu na linahitaji uangalizi ili kulitunza kwani limechakaa mno, ziwa Kyamba Ngungulu linafaa Zaidi kwa ufugaji wa samaki kutokana na msitu mkubwa uliopo, hata ufugaji wa nyuki unafaa katika eneo hili. Ziwa hili liko katika Kata ya Kambasegela.
6.8 Ziwa Lusiba
Linapatikana katika Kata ya Mpombo na ni kubwa licha ya shughuli za binadamu kuonekana kuliharibu, Halmashauri inatakiwa kuwekeza nguvu katika kurejesha hadhi ya ziwa hili. Mbali na utalii, shughuli za uvuvi pia zinaweza kufanywa katika eneo hili.
6.9 Ziwa Kyejo
Ziwa hili linapatika juu ya mlima Kyejo, lakini pia limekuwa likiharibiwa na shaghuli za binadamu. Kutoakana na hilo umeonekana kupungua. Ziwa hili ni kivutio kikubwa cha watalii.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.