MIRADI YA MAENDELEO YENYE JUMLA YA THAMANI YA SHILINGI BILIONI 6.6 YAKAGULIWA NA MBIO ZA MWENGE WA 2025 KATIKA HALMASHAURI YA BUSOKELO.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2025 Ndugu Ismail Ali Ussi ameridhishwa na usimamizi wa miradi ya maendeleo inayatokelezwa katika Halamshauri ya Wilaya ya Busokelo.Ndugu Ussi akiongoza Msafara wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo leo 10/10/2025 amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 6.6 inayotekelezwa katika Halmashauri ya Busokelo.
Miradi hiyo ni pamoja na uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa Ofisi ya Kijiji cha Kandete kata ya Kandete inayojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 59, ambapo shilingi milioni 4.16 ni mchango wa nguvu za Wananchi, shilingi milioni 55.7 zimetengwa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri.Akizungumza na Wananchi wa Kandete Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ameitaka jamii ya wakazi wa Kandete kutumia ofisi hiyo ya umma kwa ajili kutatua kero za Wananchi.
Katika hatua nyingine Ndugu Ismail Ali Ussi amewataka Wananchi wa Busokelo kushiriki katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29,2025.Aidha Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kikuba Kata ya Lufilyo wenye thamani ya shilingi milioni 149.Akiwa katika kijiji cha Kikuba kiongozi huyo wa mbio za Mwenge wa Uhuru amebainisha kuwa serikali ya Awamu ya sita inaendelea kutoa huduma bora za jamii kwa Wananchi wake ikiwemo huduma za Afya.

Miradi mingine iliyotembelewa na Mbio za Mwenge wa Uhuru ni pamoja na Uzinduzi wa Bweni la Wanafunzi katika shule ya sekondari Lwangwa wenye thamani shilingi milioni 189.7, Kikundi cha Wastarabu Bodaboda Lwangwa waliopatiwa mkopo wa shilingi milioni 16 kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri.Vilevile Mwenge wa uhuru umetembelea mradi wa ujenzi wa barabara ya Lwangwa –Kyejo yenye kilomita 6.41 kiwango cha lami iliyojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 6.19 pamoja na ugawaji wa mitungi ya kupikia yenye thamani ya shilingi 11 kwa ajili ya kuendeleza matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuhifadhi mazingira
.“Shiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu”








Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.