SHILINGI BILIONI 32.9 ZAIDHINISHWA BAJETI YA HALMASHAURI MWAKA WA FEDHA 2026/2027.
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo limeidhinisha Bajeti ya Mwaka 2026/2027 yenye kiasi cha Shilingi Bilioni 32,9 kwa ajili ya kutekeleza programu mbalimbali zilizopangwa kufanyika katika Halmashauri kwa kipindi cha mwaka huo wa fedha.

Kikao hicho cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo kimeketi leo 14/01/2026 kujadili Mapendekezo ya Mpango na Bajeti 2026/2027 kisha kuidhinisha Bajeti hiyo.
Bajeti hii imeongezeka kwa asilimia 0.47% ikilinganishwa na Bajeti ya Mwaka wa Fedha2025/2026 ambayo ilikuwa Shilingi Bilioni 32.8,
Kwa Bajeti hii Halmashauri uta punguza utegemezi
toka Serikali Kuu kutoka asilimia 11.68% mwaka 2025/2026 hadi asilimia 12.09 % Mwaka 2026/2027.
Miongoni mwa programu zinazotazimwa kutekeleza kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 ni pamoja na Ruzuku ya Mishahara (PE), Ruzuku ya Matumizi Mengineyo, utekelezaji wa Miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Fedha za Ndani (Development Local) pamoja na tekelezaji wa Miradi ya Maendeleo inayofadhiliwa na Fedha za Wafadhili (Development Foreign).
Katika hatua nyingine akiwasilisha Salamu za Serikali Katibu Tawala Wilaya ya Rungwe ,Bw.Ally S.Kiumwa amehimiza Wazazi, Walezi na Walimu kuhakikisha kuwa Wanafunzi wote waliosajiliwa kuanza Elimu ya Awali na Msingi pamoja na wale waliyofaulu kuingia Kidato cha kwanza kwa Mwaka wa Masomo 2026 kuhakikisha wote wanaripoti shuleni ili kuanza masomo yao.
Adhia Bw.Kiumwa masisitiza ni vema kuhakikisha suala la utoro kwa Wanafunzi mashuleni, linadhibitiwa ila kuwapatia Watoto Elimu Bora pamoja na kuhakikisha malengo na mikakati ya Elimu Wilayani Rungwe inafikiwa kama ilivyokusudiwa ikiwa ni pamoja kukuza ufaulu kwa Wanafunzi.
Katika Salam za Chama Cha Mapinduzi CCM Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rungwe Mhe.Meckson Mwakipunga amewashukuru Wataalamu na Halmashauri na Waheshimiwa Madiwani kwa kutekeleza Mpango huo wa Bajeti kwa zingatia Taratibu zote ikiwemo Ilani ya CCM huku akishauari Halmashauri iandike maandiko mengi(Proposals) kwa ajili ukamilishaji wa miradi mbalimbali Iliyoanzishwa kwa nguvu za Wananchi ili kuwezesha upatikana wa huduma bora kwa jamii.





Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.