Hayo yamesemwa na Wawakilishi Wakazi wa Mashirika ya UNICEF na KOICA nchini Tanzania, wakati wa ukaguzi na uzinduzi wa Miradi ya Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo.
Miradi hiyo inayofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea (KOICA), ambapo wametoa fedha kwa ajili ya Ujenzi na Ukarabati wa Majengo pamoja na Vifaa kwa ajili ya huduma za afya ya uzazi na huduma kwa motto katika Zahanati na Vituo vya afya Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Maeneo waliyotembelea ni pamoja na Kijiji cha Nsanga kukagua na kutoa huduma za Mkoba za uzazi nz motto, Zahanati ya Kambasegela kuzindua jingo lahuduma ya afya ya uzazi na mtoto na Kituo cha Afya cha Mwakaleli ambapo walizindua jengo la wodi ya wazazi.
Bi. Maniza Zaman ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la UNICEF – Tanzania, alisema kuwa anayo furaha kuona kuwa malengo ya kuhudumia afya ya mzazi na mtoto inafanikiwa. Naye Bi. Hyunsun Kim ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la KOICA – Tanzania, alisema kuwa katika nchi ya Korea wanatoza kiasi cha fedha dola 1 za Marekani kwa kila abiria anayetumia usafiri wa ndege ili kuchangia fedha kwa
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.