Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. KassimMajaliwa amewataka Watendaji na Watumishi wa Umma wa Halmashauri yaWilaya ya Busokelo kuwatumikia Wananchi wake kikamilifu. Akiongea katikaMkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Kandete, alisema kuwa Watumishiwa umma wanapaswa kwenda kule waliko Wananchi ili kutatua kero mbalimbaliambazo wanakabiliwa nazo na sio kukaa Ofisini tu.
Akaongeza kuwa Serikali imetoa fedha za Miradi mbalimbali kwaWananchi na Watendaji wa Serikali wanapaswa kusimamia kwa karibu matumizi yafedha hizo. Fedha zimetolewa kwa miradi ya Maji (Mipya na zamani) namiundombinu ya barabara na madaraja.
Aidha alisema kuwa Serikali inakusudia kutengeneza barabara yaKatumba – Mwakaleli – Lwangwa – Mbambo – Tukuyu kwa kiwango cha lami nakuimarisha barabara ya Mbambo-Ipinda kwa kiwango cha Changarawe, barabara hizizitachochea maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.