BUSOKELO KUWAPATIA WATOTO CHANJO YA POLIO.
Kampeni Kitaifa ya chanjo ya polio itafanyika nyumba kwa nyumba katika Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo ili kuwakinga Watoto wote walio na umri 0 hadi miaka 8 dhidhi ya ugonjwa hatari wa Polio.
Hayo yamebainishwa leo 18/09/2023 na Mwenyekiti wa Kamati ya Msingi ya Afya ngazi ya Jamii Mhe. Jafarr Haniu katika kikao kilicho wakutanisha wajumbe wa kamati hiyo katika Ukumbi wa Halmahsauri ya Wilaya ya Busokelo Kwa ajili ya maandalizi ya kampeni ya Kitaifa ya Chanjo ya Polio itakayo anzaa tarehe 21-24/09/2023
Akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa kamati hiyo Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe. Jaffar Haniu, amewaagiza wajumbe wa kamati wahakikishe kuwa jamii inashirikishwa kikamilifu, ili zoezi la utoaji chanjo ya matone ya Polio iwafikie kwa wingi watoto katika maeneo yote ya Busokelo.
“Nikampeni ya Kitaifa ambayo itaanza kuanzia 21 mpaka tarehe 24, itahususha Watoto wenye umri wa miaka 0 hadi 8, itahusisha vituo vya afya,maeneo ya mikusanyiko, nyumba hadi nyumba, ni zoezi amabalo linahitaji ushiriki wetu sote , viongozi wa dini Watumishi kwahiyo niwaombe sana tushiriki kila mmoja kwa nafasi yake lengo Watoto wapate chanjo ili tuweze kuwakinga Watoto wetu dhidhi ungonjwa huu ” amesema Mhe.Haniu.
Akifafanua kuhusu kampeni ya kitaifa ya Chanjo ya Polio, Mratibu wa Chanjo Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo Bw. Bariki Mhagama ameeleza kuwa lengo la Kampeni hiyo ni kuongeza uelewa kwa wanajamii kuhusu faida ya chanjo za Polio, Kuwafikia watoto wengi zaidi katika maeneo yetu na taasisi zetu, kutumia taasisi, taaaluma na nafasi tulizonazo ili kuwafikia wanajamii kwa kauli moja ya kwenda kuwapeleka Watoto wapate chanjo itakayo wakinga dhidhi ya ugonjwa wa Polio na kuwa Mabalozi wa kuendesha kampeni dhidi ugonjwa hatari wa Polio na chanjo yake.
POLIO ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi cha polio, ugonjwa huu humsababishia mgonjwa kupooza viungo vya mwili na hata kupoteza maisha. Virusi vinaweza kuingia kwa njia ya mdomo kwa kunywa maji au chakula ambacho kimechafuliwa na kinyesi kutoka kwa mtu aliyeambukizwa na virusi hivyo
Kwa mara ya mwisho Tanzania ilipata Mgonjwa wa Polio mnamo mwaka 1996 ,hivi karibuni Mgonjwa amegundulika Sumbawanga Mkoani Rukwa, na hivyo Serikali imeamua kufanya kampeni ya chanjo ya Polio katika mikoa ya Rukwa, Mbeya, Songwe, Katavi, Kigoma na Kagera.
Walengwa wa chanjo ya watoto walio na umri 0 hadi miaka 8 walioko mashuleni, Nyumbani, Vituo vya kulelea watoto, na shule za awali bila malipo yoyote.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.