Kamati ya BOOST YA HALMASHAURI, Leo tarehe 04.04.2023 imekutana na viongozi wa kata, vijiji na Shule kwa maeneo yaliyopata miradi na kuwajulisha kiasi cha fedha zilizopokelewa pamoja na taratibu, muda wa utekelezaji, uundwaji wa kamati tatu ndogo pamoja na majukumu yao
Mratibu wa Mradi Mwalimu Darus Limandola amewaeleza wajumbe Shule zilizopata mradi wa BOOST ikiwa ni pamoja na:-
1.Ipoma shule ya msingi madarasa 2 ya Elimu ya awali yenye thanani yaTZS.69.1milioni
2.Kandate shule ya msingi madarasa 2 ya kawaida yenye thanani ya TZS 50Mil na vyoo matundu 3 yenye thamani ya TZS 6mil
3. Kingili shule ya msingi madarasa 3 ya kawaida yenye thanani ya TZS 75mil na vyoo matundu 3 yenye thanani ya TZS 6mil
4. Mbambo shule ya msingi madarasa 2 ya kawaida yenye thanani ya TZS 50mil na vyoo matundu 3 yenye thanani yaTZS 6mil
5. Ndobo shule ya msingi madarasa 2 ya kawaida yenye thanani ya TZS 50 mil na vyoo matundu 3 yenye thanani ya TZS 6 mil
6. Lwangwa shule ya msingi ujenzi wa shule mpya ya mkondo mmoja TZS 347.5mil
Aidha wajumbe wamepewa muda wa utekelezaji wa miradi ni wa siku tisini kuanzia tarehe 27.03.2023 pamoja na maelekezo mengine kama ifuatavyo
1. Wameelezwa malengo ya miradi ya BOOST
2. Mpango wa utekelezaji wa siku 90, kwa Halmashauri ni siku 80 kwa ngazi ya shule
3.Umuhimu wa vikao vya kila wiki ngazi ya shule kwa ajili ya utekelezaji wa mradi na kujua hatua ya ujenzi
4.Uandishi wa mihtasari wa vikao
5.Nyaraka mbalimbali na utunzaji wa nyaraka hizo
6.Wajibu wa wananchi katika ulinzi na umilikaji wa mradi na uwazi wa matumizi ya fedha
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.