DC HANIU ATEMBELEA KALAKANA ZILIZOPO CHUO CHA VETA BUSOKELO.
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe.Jaffar Haniu leo 01/03/2025 amekagua kalakana za ufundi zilzipo katika chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA-BUSOKELO kilichopo kijiji cha Kifunda kata ya Lufilyo Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo.
Mhe.Haniu akiwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya miaka 30 ya kuundwa kwa VETA na miaka 50 ya utekelezaji wa Mafunzo ya Ufundi Stadi yaliyofanyika katika chuo cha VETA-BUSOKELO.
Akiwa chuoni hapo Mhe.Haniu alikagua Kalakana ya Ufundi umeme, Kalakana ya Ufundi selemala pamoja na kalakana ya ushonaji nguo.
Aidha Mhe Haniu alizindua programu ya mafunzo ya uendeshi pikipiki kwa vijana wa Bodaboda program inayolenga kuwajengea ujuzi wa kuenda Bodaboda vijana kwa lengo kupunguza ajali barabarani.
Katika hatua nyingine Mhe.Haniu ameutaka uongozi wa Chuo cha VETYA BUSOKELO kuanzisha program za mafunzo ya kilimo cha kisasa na ufugaji wa samaki ili kuwawezesha vijana kuchwamua kiuchumi kupitia kilimo cha kisasa na ufugaji.
Pia Mhe.Haniu amezindua kampeni ya uchangiaji Damu salama katika maadhmisho hayo VETA kwa lengo kuoka maisha ya Wagonjwa wenye uhitaji wa damu katika vito vya kutolea huduma za afya.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.