ELIMU KUHUSU UMUHIMU WA BIMA YA AFYA YA iCHF ITOLEWE ZAIDI KWA WANANCHI WA BOSOKELO.
NA PETER TUNGU.
Katika Kuboresha utowaji wa huduma za afya kwa wananchi wa Busokelo, Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo Mkoa wa Mbeya limewaagiza Watumishi wa Idara ya afya Busokelo waendelee kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa Bima ya Afya iliyo rahisishwa iCHF ili kuwahamasisha wananchi wengi kujiunga katika bima ya iCHF kwaajili ya kupatiwa matibabu katika vituo vya kutoelwa huduma za afya vinavyo patikana katika Halmashauri ya Busokelo.
Hayo yameelezwa katika Kikao cha robo ya nne 2022/2023 cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo kilichofanyika leo tarahe 02/08/2023 katika ukumbi mpya wa mikutano wa Halmashauri hiyo kikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe.Anyosisye Njobelo na kuhudhuria na wajumbe Waheshimiwa madiwani wa kata na Viti maalamu, na wataalamu kutoka Halmashauri ya wilaya Busokelo akichangia hoja kuhusu kamati ya fedha na mipango katika suala la ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri ,Diwani wa viti maalum CCM Mhe. Essah J.Msiku aliwashauri wataalamu wa idara ya Afya Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo waendelee zaidi kutoa eilimu kwa Wananchi wa Busokelo hasa maeneo ya vijijini kuhusu umuhimu wa Bima ya afya ya iCHF ili kupata wanachama wengi zaidi katika mfuko huo na wananchi waweze kupata huduma za afya kwa urahisi hasa waishio katika maeneo ya vijijini. “ukiangalia kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwenye chanzo cheti cha iCHF tulikuwa na aslimia 81% lakini kwa mwaka fedha 2022/2023 tumefikia asilimia 91.29% nitume nafasi hii kumpongeza Mkurgenzi na kamati kwa usimamizi mzuri, nipende kushauri kuongeza bidii na juhudi kwa wananchi ili waendelee kujiunga na ili tuweze kuongeza mapato na wananchi waweze kufaidika nah ii huduma” amesema Mhe. Msiku.
Bima ya Afya ya Jamii iliyoboreshwa iCHF ni Bima ya Afya iliyoanzishwa na serikali ya Tanzania chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi kwa kushirikiana na Wizara ya Afya amabapo huduma za matibabu hutolewa kwa mwanachama mwenye kadi ya CHF kuanzia Zahanati, Kituo cha Afya , Hospitali za Wilaya na Mikoa kwa nchi nzima.
Aidha katika hatua nyingine Diwani wa Kata ya Mpata Mhe.Mekara O.Mwangombola alihoji ni lini serikali itahakikisha kila Kijiji kinakuwa na Zahanati ikwemo Kijiji cha Ipagika kilichopo katika Halmahsuari ya Busokelo Mkoa wa Mbeya.
Akijibu swali hilo Mwenyikiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo Mhe. Anyosisye Njobelo alisema kuwa jukumu la kujenga zahanati ni jukumu la wanakijiji na Serikali huwaunga mkono wanakijiji katika hatua hiyo. “Mwongozo unaelekeza kuwa kila kata iwe na kituo cha afya na kila kijiji kiwe na Zahanati, sasa kuanziasha zahanati siyo serikali kinaanzisha kijiji ndiyo serikali unawaunga mkono, sasa wana Ipagika kawaambie Serikali inataka wawe na mahali pakujenga,watenge eneo lipimwe litambulike kisheria halafu pale ndiyo waanzishe zahanati na serikali itwaaunga mkono” alisema Mhe.Njobelo,
Naye katibu wa Baraza la Madiwani ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo Mhe.Loema I.Peter alisema kuwa katika utekelezaji ujenzi miradi ya afya, Halmashauri hutenga fedha kwaajili ya ukamilishaji maboma ambayo wananchi wameyajenga “Katika bajeti ya Halmashauri huwa tunatengea bajeti ya maboma ambayo wananchi wamekwisha jenga, Serikali inatengea bajeti kwaajili ya kumalizia maboma hayo na tumefanya hivyo kwa miaka kadhaa,ni maboma kadhaa yameshaletewa fedha katika upande wa afya na elimu pia, mfano halisi mwaka uliyopita tulipokea ukamilishaji wa maboma nane(8) ya zahanati ,kila boma lilitengewa milioni 75 ,na utaratibu ni uleule Mheshimiwa Mwenyekiti kwa hiyo wananchi wao waendelee kujenga maboma kwa wingi, kila tutakapo andaa bajeti tutakuwa tunatenga kwajili ya kukamilisha hayo maboma’’ alisema Mhe. Loema.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.