FUM YAAGIZA MRADI WA MAWESE KISEGESE UZALISHAJI UANZE.
Na Peter I.Tungu.
Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango (FUM) Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, imekagua mradi wa kikundi cha akina Mama cha kuchakata mawese kilichopo katika kata ya Kisegese ikiagiza mradi huo ukamilike ili kuanza uzalishaji wa mafuta ya mawese.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, Mhe. Anyosisye Njobero, aliongoza ziara hiyo tarehe 18/07/2023 akiwa na Mkurugenzi Mtendji Halmashauri ya Busokelo Mhe.Loema I.Peter ambaye ndiye katibu wa kamati ya (FUM), pamoja na wajumbe wa kamati hiyo ambao ni Waheshimiwa Madiwani na Wakuu wa Idara na vitengo Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, kwaajili ya kufanya tathmini ya miradi ya maendeleo ya jamii inayotekelezwa katika Halmashauri ya Busokelo.
Mradi huo wa akinamama wa Kukamua mawese katika kata ya Kisegese, unajumuisha wanawake watano(5), upo katika hatua ya ufungaji mitambo una gharama ya milioni 25, ambazo zimetokana na mkopo unaotolewa na Halmashauri kwaajili ya kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 22/07/2027.
Aidha Mwenyekiti wa kamati ya (FUM) alipongeza kazi nzuri iliyofanywa na wanakikundi hao, akiwataka wakamilishe kwa haraka ufungaji wa mashine na uzalishaji uanze mara moja ili wanakikundi waanze kurejesha mkopo.Katika hatua nyingine Mhe.Njobero amewashauri wanakikundi hao kujenga stoo kwaajili ya kuhifadhi mafuta watakayo zalisha kiwandani hapo. “niwapi mmetenga eneo la stoo kwaajili ya kuhifadhi bidhaa zenu, ni vema basi mradi ukikamilika mjenge stoo kwaajili ya kuhifadhi mafuta mtakayo zalisha,ni lazima kuwe na stoo” amesema Mhe. Njobero.
Awali akisoma taarifa ya wanakikundi, Katibu wa mradi hou Bi.Rosa Kalesa,alisema mpaka sasa Kikundi kimefanikiwa kununua mshine mbili kwaajili ya kukamulia mawese zenye thamani ya shilingi million 13, million 12 zikitumika katika ujenzi wa jengo la mradi, gharama za ufundi na usafirishaji vifaa vya ujenzi.Naye Diwani wa kata ya Kisegese Mhe Losajo K.Brayan aliwapongeza wanakikundi hao kwa hatua waliyofikia katika utekelezaji mradi, huku akisisitiza kuwa anatamani kuona kazi hiyo ikikamilika haraka ili uzalishaji uanze katika eneo la mradi.
Mradi wa kukamua mawese Kisegese ulitarajiwa kukamilika tarehe 17/07/2023, hivyo mafundi wanangojea kukauka kwa zege katika eneo ambalo mashine zinararajiwa kufungwa. Hivyo kamati ya (FUM) aliagiza hadi kufikia tarehe 22/07/2023 mradi uwe umekamilika na uzalishaji uanze.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.