HALMASHAURI 7 ZA MKOA WA MBEYA ZAPATIWA MAFUNZO YA MATUMIZI YA MFUMO WA MANUNUZI YA UMMA KWA NJIA YA MTANDAO NeST.
Mafunzo hayo ya siku tano yenye lengo la kuwajenga uwezo Maafisa wa Serikali Watumishi wa Umma juu ya namna bora ya kutumia Mfumo mpya wa serikali wa Manunuzi ya Umma kwa njia ya mtandao NeST yamehusisha Maafisa Manunuzi, Wakaguzi wa ndani,Wanasheria Maafisa TEHAMA, Maafisa Mipango na Maafisa Habari kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, Chunya, Mbeya Mbalali, Kyela, Rungwe, Mbeya vijijini na Mbeya Jiji.
Mafunzo hayo yameanza jana tarehe 23/08/2023 katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, yanatarajiwa kukamilika ifika tarehe 27/08/2023.
Akizungumza katika Mafunzo hayo Mkufunzi wa matumizi ya Mfumo wa NeST, Afisa TEHAMA Mkoa wa Mbeya Bwana Frank Choka amewataka washiriki wote kufuatilia na kuzingatia mafunzo hayo kwa weledi ili wakawe Mabalozi wazuri katika maeneo yao ya kazi kwa kuwafundisha watumishi na watu wengine kuhusu namna bora ya kutumia Mfumo wa NeST katika manununzi ya Umma.
Serikali ya Tanzania ilitambulisha mfumo mpya wa manunuzi ya Umma kwa njia ya Mtandao NeST katika mwaka wa fedha 2023/2024, kutoka katika mfumo wa zamani ujulikanao kama TANEPS.
Mfumo mpya wa Ununuzi NeST unatarajiwa kuanza rasmi katika Taasisi zote za Umma ifikapo Octoba Mosi 2023.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.