JAMII IJENGEWE UELEWA KUHUSU UMHIMU WA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA 2024.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Bw.Ramadhan Kailima amewataka Maafisa Habari na Mikoa na Halmashauri nchini kuhakikisha jamii ya Watanzania inajengewa uelewa kuhusu umuhimu wa Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura mwaka 2024.
Bw.Kailima emeeleza hayo leo 15/06/2024 katika Mkutano wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dares Salaam.
Bw.Kailima amesema kuwa Maafisa Habari Kwa kushurikiana na vyombo mbalimbali vya Habari vilivyopo katika Mikoa na Halmashauri wanao wajibu wa kuueleimisha Umma wa WaTanzania kuhusu zoezi la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura kwa kutoa taarifa sahihi na kupinga aina yoyote ya upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya watu katika jamii.
Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura nchini linatarajiwa kuzinduliwa rasmi July 1/2024 Kitaifa Mkoani Kigoma.
Kwa kuzingatia matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi, Wapiga Kura wapya 5,586,433 wanatarajiwa kuandikishwa ambao ni sawa na asilimia 18.7 ya Wapiga Kura 29,754,699 waliopo kwenye Daftari la baada a Uboreshaji uliofanyika Mwaka 2019/2020.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura Bi.Giveness Aswile amesema kuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi NEC, Kwa kuzingatia mashariti ya kifungu cha 9(1) na (2) cha sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na ya Mwaka 2024 pamoja na vifungu vingine vinavyohusu uandikishaji na Uboreshaji, zoezi hilo lina husisha mambo muhimu mambayo ni:
1.Kuandikisha Wapiga Kura wapya amabo ni Raia wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na zaidi na watakao timiza umri huo ifikapo tarehe ya Uchaguzi Mwaka 2024.
2.Kutoa fursa Kwa Wapiga Kura waliopo kwenye Daftari na ambao wamehama, ili waweze kuhamisha taarifa zao kutoka kata au Jimbo walilonandikiashwa awali.
3. Kutoa fursa Kwa Wapiga Kura walilonandikiashwa kurekebisha taarifa zao yakiwemo majina na taarifa nyingine.
4. Kuotoa kadi mpya Kwa Wapiga Kura Walipoteza kadi au kurekebisha kadi zao zilizo haribika
5. Kuondoa taarifa ya Wapiga Kura Walipoteza sifa za kuwepo kwenye Daftari la kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuukana uraia wao wa Tanzania au kifo.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.