Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Mhe. Julius Chalya wakati wa uzinduzi wa jukwaa la uwezeshaji wanawake Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Uzinduzi wa jukwaa hilo ulienda sambamba na maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ikiwa na kaulimbiu ya “Kuelekea uchumi wa Viwanda, kuimarisha usawa wa jinsia na uwezeshaji wa wanawake Vijijini”.
Alisisitiza kuwa wanawake lazima waunde vikundi vitakavyowawezesha kupata mikopo na kuzalisha bidhaa zitakazo wapatia kipato kwa kuongeza thamani ya bidhaa hizo.
Serikali iliahidi kuleta milioni hamsini kwa kila kijiji lakini haikumaanisha kuwa italeta fedha kwa kila mtu kumbe badala yake fedha inakuja kwa watu waliojiandaa ikiwa na maana kutoa mikopo kwa makundi na kufanya uzalishaji utakaoinua uchumi wa kila mmoja.
Vikundi hivi vikishaundwa vipewe elimu ya uzalishaji mali wenye tija, ili wazalishe bidhaa zenye ushindani katika masoko na kuweza kuinua uchumi wa wananchi. Wapewe elimu lakini pia waunganishwe Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) ili wapewe elimu za uzalishaji na vifungashio.
Wakishukuru wanawake hao walisema kuwa wanafurahi kwa kuwa sasa wana jukwaa la kusemea mambo yao, kwani sasa wanaona njia ya kupata mafanikio ya kuinuka kiuchumi ipo jirani na shughuli zao.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.