Kituo cha radio cha Kyela FM kupia kampeni yake ya “Na mimi Nimo” kimetoa hamasa kwa kushiriki usafi unaofanyika kila jumamosi ya kila mwisho wa mwezi. Katika kampeni hii Kituo hicho cha redio kwa kushirikiana na wadau wao wa Songoro Marine na Kyela Polytechnic College “KPC” kiliungana na wakazi wa Kata ya Kandete iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo katika kufanya usafi katika kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Hivyo baada ya usafi, wadau walikabidhi msaada wa sabuni za kufulia kwa wagonjwa waliolazwa katika kituo cha Afya cha Mwakaleli.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.