KAMPUNI YA UJENZI WA BARABARA YA CHINA ROADS AND BRIDGE CO-OPERATION YASAINI MKATABA WA KUWA MPANGAJI KATIKA MAKAMBI YA MBAMBO.
kampuni ya Ujenzi wa Barabara ya CHINA ROADS AND BRIDGE CO-OPERATION kutoka Uchina leo 29/05/2025 imesaini Mkatabata wa kuwa mpangaji katika Makambi ya Ujenzi wa Barabara yaliyoko Kijiji cha Mbambo Kata ya Kambasegela.
Zoezi la utiaji saini limefanyika leo katika shule ya msingi Mbambo Kata ya Kambasegela likiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo Mhe.Anyosisye Njobelo na kusimamiwa na Mwanasheria wa Halmashauri ya Busokelo Wakili Peter Salama.
Kampuni hiyo imeingia Mkataba wa miaka minne (04) kama mpangaji katika makambi ya Mbambo ambapo zoezila utiaji saini Mkataba huo limeshuhudiwa pia Viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Mbambo, baadhi ya Wananchi pamoja Mhe .Diwani ya Kata ya Kambasegela.
Akuzungumza katika Hafla hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Busokelo Mhe.Anyosisye Njobelo Wananchi wa Mbambo na Kambasegela kwa ujumla kuwapokea wageni hao kwa ukarimu.
Adha Mhe.Njobelo ameleza kuwa ni marufuku watoto wote wakiwemo Wanafunzi kuingia katika makambi hayo ili kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto ikiwemo vitendo vya ulawiti na ubakaji.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.