Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo imetoa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na walemavu ili kukuza mitaji na kuinua uchumi na kipato kwa jamii. Fedha hizi ni utekelezaji wa maagizo ya serikali kwa kila halmashauri kutenga fedha 10% kwa ajili ya wanawake, vijana na walemavu.
Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi za mikopo zenye thamani ya shilingi milioni 32 kwa vikundi hivyo iliyofanyika kwenye jengo la soko la ndizi Lupata Januari 25 mwaka huu, Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Mhe. Julius Chalya alisema kuwa umefika wakati ambao sasa wananchi wanatakiwa kuunda vikundi ili kunufaika na mikopo kutoka serikalini.
“Kuna watu wamekuwa wakilalamika kuwa Serikali haiwawezeshi kiuchumi wakati hawataki kujiunga katika vikundi. Serikali haiwezi kumpelekea fedha kila mmoja mahali alipo, tengenezeni vikundi ili mnufaike na fursa hizi”. Alisema Mhe. Chalya
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.