Maafisa Waandikishaji Wasaidizi Ngazi ya Kata katika Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo leo 19/12/2024 wamekula kiapo cha siri na Kujitoa Uanachama wa Siasa mbele ya ya Hakimu Mkazi Mahakama ya Ikama Mhe.Chuma Vestadus Mataba ikiwa ni maandalizi kuelekea zoezi la Uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linalotarajia kuanza 27/12/2024 hadi 02/01/2025.
Jumla ya Maafisa Waandikakishaji Wasaidizi 13 kutoka kata zote za Busokelo wamekula kiapo hicho katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo.
"Kujiandikisha kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora"
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.