Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila amewaasa wataalam na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo kubuni vyanzo vipya vya mapato ambavyo havitaathiri wananchi.
Akiyaongea hayo jana katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo la kujadili hoja za ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2016/17 lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Busokelo.
“Nashauri au nawashauri kuendelea kufanya utafiti wa vyanzo vipya vya mapato ambavyo havitawaathiri wananchi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali vitakavyoziba pengo la kuongezeka kwa mapato” Alisema Chalamila.
Mhe. Chalamila alisema kuwa anawaagiza wataalam kufanya uchmbuzi wa kina wa vyanzo vyote vya mapato ili kuwa na takwimu sahihi za kila chanzo ili kuwa na makadilio sahihi kwa kila chanzo hivyo kuwa na mapato yanayopanda na sio kushuka.
Aidha aliagiza kuwa halmasahuri inapaswa kusimamia vyanzo vyote vya mapato ipasavyo na pia kukusanya mapato kwa kutumia mashine za kielektroniki za kukusanyia mapato (POS) ili kudhibiti mianya ya uvujaji wa mapato.
Baraza la Madiwani la Halimashauri ya Wilaya ya Busokelo la kujadili hoja za ukaguzi za Mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali linaloongozwa na Mkuu wa Mkoa hukaliwa kila mwaka ili kujadili hoja za hesabu kwa mwaka fedha uliopita ambapo kwa miaka 3 mfululizo halmashauri ya Wilaya ya Busokelo imeendelea kupata hati inayoridhisha.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.