Katibu Tawala wa Wilayaya Rungwe, Bw. Nnkondo Bendera amewataka watumishi wa Wilaya ya Busokelo kubadilika kiutendaji kulingana na wakati.
Aliyaongea hayo jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Busokelo wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani wakati wa kujadili taarifa za robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2018/19.
“Sasa tumehama kutoka kwenye uongozi wa maneno….kwenda kwenye uongozi wa matokeo…. tunaita ‘Result based Management’ na kwamba kila mmoja lazima awe na KPI (Key Perfomance Indicators) kwenye utumishi wake” Alisema Bw. Bendera
Bw. Bendera aliongeza kuwa lazima kuwe na mipango na mipango hiyo itengenezewe shughuli za utekelezaji na pia zionyeshe kuwa zinakwenda kutatua tatizo fulani kwenye jamii.
“Hili nimeongea na Mhe. Mkuu wa Wilaya kwamba itafikia hatua tutakaa na Wataalamu wote wa Wilaya ya Rungwe na kuingia nao mkataba wa kiutendaji ili tujue tunapigaje hatua, kwamba Rungwe tulukuwa wapi na sasa tupo wapi”. Alisema Bw. Bendera
Aliongeza kuwa tunatakiwa tujifunze kutoka kwa wenzetu nchi ya Malaysia ambako tulichukuwa mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Result Now) ambapo wao kwa sasa mtu akijipima mwenyewe kuwa hatoshi hawezi kuchukua uongozi ili awaachie ambao wanaweza kuleta matokeo chanya kwa jamii.
Bw. Nnkondo Bendera alipata wasaa wa kuyasema haya kwenye Baraza la Madiwani Busokelo ikiwa ni sehemu ya taarifa kutoka Serikali Kuu pia ikiwa ni sehemu ya kujitambulisha kwa Madiwani hao kwani ni Baraza lake la kwanza kuhudhuria tangu alipoteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Rungwe.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.