Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2018, Ndg. Charles Francis Kabeho amesema kuwa umefika wakati Watanzania kuwa na utaratibu wa kupima Afya zao.
Aliyasema hayo jana katika viwanja vya soko la Ntangasale, Kata ya Kabula wilayani Busokelo wakati wa kutoa ujumbe wa Mwenge wa uhuru baada ya kukimbizwa na kuzindua miradi mbambali ya maendeleo yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.2
“Tunatakiwa kupima afya zetu ili kuzijua hali zetu, Serikali imewekeza kwenye afya na dawa za kupunguza makali ya VVU zipo za kutosha”. Alisema Kabeho
Aliongeza kuwa Taifa lolote linahitaji watu wenye afya na nguvu ili kuleta maendeleo ya nchi na kwa Taifa letu wanahitajika watu wenye afya ili kujenga Taifa imara kuelekea uchumi wa viwanda.
Mbio za mwenge wa uhuru 2018 ikiwa na kauli mbiu ya “Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu” zilizinduliwa rasmi mwezi Aprili, 2018 mkoani Geita na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na utakimbizwa katika halmashauri zote 195 za Tanzania kabla ya kuhitimishwa kwa mbio hizo mnamo Oktoba 14, 2018 Mkoani Tanga.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.