MAADHIMISHO YA JUMA LA ELIMU YA WATU WAZIMA 2023 MKOANI MBEYA
Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo imeshiriki maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima kimkoa yaliyofunguliwa rasmi leo 25 Septemba 2023 Wilayani Mbarali na kuhudhuriwa na Wakuu wa Idara mbalimbali, na wenyeviti wa Kamati za Huduma ya Jamii kutoka Halmashauri zote 7 za Mkoa wa Mbeya.
Maadhimisho hayo yaliyoongozwa na Kauli mbiu isemayo " Kukuza uwezo wa Kusoma na kuandika kwa ulimwengu unaobadilika; Kujenga misingi ya Jamii endelevu na yenye amani" yamezinduliwa rasmi tarehe 25/09/2023 Katika Kiwanda cha Kuzalisha taulo za kike IPOSA kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.
Katika Maadhimisho hayo, Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii Halmshauri ya Wilaya ya Busokelo ambaye ni Diwani wa Kata ya Ipagika Mhe.Mekara O.Mwang'ombola, alipongeza juhudi zilifanywa na Idara ya Elimu ya Watu wazima Halmshauri ya Mbarali kuwaweshea vijana wa kitanzania kupata mafunzo ya ufundi stadi kuhusu namna ya Utengenezaji taulo za kike katika kiwanda cha IPOSA kilichopo Mbarali kwani hii ni njia mojawapo ya kuwajengea ujuzi na maarifa vijana katika jamii ili waweze kuwa na uwezo wa kujiajiri wenywe na kujiingizia kipato.
Mhe.Mekara aliahidi kuwa, Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo pia itendelea kuwawezesha vijana kwa kuwajengea uwezo ktk mafunzo mbalimbalj ya Ujasiriamali ili waondokane na utegemezi kwa kujiingizia kipato kupitia fursa mbalimbali zitakazo patikana baada ya mafunzo wanayopatiwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo.
Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima nchini hufanyika kila Septemba ya kila mwaka tangu yalipoasisiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) mwaka 1966 na kuanza kuadhimishwa rasmi mwaka 1967 chini ya Uongozi wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.