Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Busokelo akitoa neno juu ya maadhimisho ya siku ya Afya na lishe katika kijiji cha lukasi kilichopo Halmashauri ya Busokelo kata ya lwangwa.
Kaimu huyo aliambatana na kamati ya lishe wilaya ili kujionea shughuli zinazofanyika katika siku hii aidha Kaimu huyu alisisitiza wananchi kua kuweza kuhudhuria siku hii ili kujipatia Elimu ya lishe na Afya kiujumla.
Kaimu Mkurugenzi pia aliomba wananchi wa walukasi kuhakikisha wanachangia vyakula shuleni ili watoto waweze kupata chakula shuleni na hivyo kuinua Taaluma yao kiujumla.
Wakati huo Afisa lishe Busokelo Bi Mwanahawa Ntandu alisisitiza mlo kamili kwa kufuata makundi matano ya chakula na pia aliwaomba wananchi kwa pamoja kutokomeza udumavu kwa kua makini katika siku 1000 ambazo zinaanzia kipindi mama akiwa mjamzito hadi miaka miwili ya mtoto.
Siku hizi 1000 ni muhimu katika ukuaji na maendeleo ya mtoto kiujumla .
Pia alitoa wito kwa wale wanaokosa siku hii kwani hukosa siku muhimu na huduma zitolewa siku hii ni Elimu ya lishe, Elimu ya bustani jiko na ufugaji wa wanyama wadogo wadogo , elimu ya usafi , maendeleo na ustawi wa jamii lakini pia upimaji wa hali za lishe, ugawaji matone ya vitamini A na dawa za minyoo pamoja dawa za kuongeza wekundu wa damu kwa kina Mama.
Upikaji wa vyakula mchanganyiko kwa watoto ambao utahusisha makundi mbalimbali ya chakula .
Hivyo alisisitiza ni siku isiyo yakukosa kwa jinsia zote.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.