MAAFISA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NGAZI YA KATA JIMBO LA BUSOKELO WAPITWA MAFUNZO KUELEKEA ZEOZI LA UBORESHAJI DAFATARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA..
Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata katika Jimbo la Busokelo wameanza mafunzo Kuelekea zoezi la Uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga kura linatarajia kuanza 27/12/2024 hadi 02/01/2025.
Akifungua Mafunzo hayo ya siku mbili leo 19/12/2024
Afisa Mwandikishaji Jimbo la Busokelo Adv.Peter Salama Mwakasonge, amewataka Washiriki wa mafunzo hayo kujifunza kwa umakini kupitia mafunzo ya nadharia na vitendo kwa muda wa siku mbili kuanzia leo 19/12/2024 hadi 20/12/2024 kisha kwenda kutekeleza jukumu la Uboreshaji Daftari Kudumu la Wapiga kura kwa weledi ifikapo 27/12/2024
Aidha Adv.Salama amesisitiza kuzingatiwa kwa Sheria, kanuni na miongozi iliyoweka katika kutekeleza zoezi la uandikishaji.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 16 (5) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024, Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utakuwa mara mbili kati ya kipindi kinachoanza mara baada ya uchaguzi mkuu na kabla ya siku ya uteuzi. Wanaohusika katika zoezi hili ni wananchi ambao: -
Wametimiza umri wa miaka 18 na kuendelea ambao hawakuandikishwa hapo awali;
Watakaotimiza miaka 18 kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
Waliojiandikisha awali na wamehama Kata au Jimbo moja kwenda jingine.
Waliopoteza sifa mfano wale waliofariki kuondolewa katika Daftari.
Wenye taarifa zilizokosewa wakati wa uandikishaji; na
Waliopoteza au kadi zao kuharibika.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.