Halmashauri inajitosheleza kwa chakula, ambapo mahitaji ya chakula kwa wakazi wote wa Busokelo ni tani 2,798 kwa mwezi na tani 33,576 kwa mwaka.
Aidha malengo ya uzalishaji wa mazao ya chakula kwa mwaka 2024/2025 ni tani 355,232.7 ambapo kwa kipindi Julai hadi Disemba 2024, tani 201,249.5 za chakula zimezalishwa na kusababisha ziada ya tani 153,983.2.
Sekta ya kilimo inaongoza kwa kutoa ajira kwa wakazi wengi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokeo na nje ya Halmashauri.
Halmasauri kupitia Divisheni ya Kilimo , Mifugo na Uvuvi inashirikia na wakulima kuwapatia ushauri wa kitaalamu, Wakulima wanaopata huduma za ugani wameongezeka kutoka Wakulima 18,956 mwaka 2020 na kufikia 54,952 Disemba, 2024.
Uwiano wa wakulima wanaotumia mbolea za viwandani umeongezeka 76% mwaka 2020 kufikia 96% kufikia Disemba, 2024.
Wastani wa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara umeongezeka kuanzia mwezi Disemba,2024 uzalishaji wa mahindi umefikia tani 8,345.
Hadi kufikia mwezi Disemba,2024 uzalishaji wa Ndizi umefikia tani 80,421
Uzalishaji wa mpunga umeongezeka hadi kufikia tani 9113 kwa mwezi Disemba, 2024 kutoka tani 8,112 kwa mwaka 2020
Uzalishaji wa viazi mviringo umeongezeka hadi kufikia tani 62470.5 mwaka Disemba, 2024 kutoka tani 32,544 mwaka 2020.
Uzalishaji wa magimbi umeongezeka hadi kufikia tani 40,90 mwezi Disemba, 2024 kutoka tani 38,325 mwaka 2020.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.