ELIMU YAHATUA ZA KUWASILISHA MALALAMIKO KWA WATUMIAJI WA TAASISI ZA KIFEDHA.
Benki Kuu ya Tanzania imewapatia Elimu Watumishi wa Umma katika Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo namna ya kutumia Mfumo wa kuwasilisha malalamiko kuhusu Taasisi za Kifedha.
Mafunzo hayo yamefanyika leo 21, Machi 2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Busokelo.
Lengo la matumizi ya Mfumo huo ni kuwezesha kurahisisha utatuzi wa malalamiko ya watumiaji wa Taasisi za Kifedha ikiwemo Benki na Taasis ndogo za utoaji huduma za kifedha wasiyochukua Amana Microphinance
Maafisa wa Benki kuu ya Tanzania BOT Kanda ya Mbeya , wamewataka Watumishi wote wa Umma na wateja wote wa Taasisi za Kifedha kuhakikisha wanasoma kwa makini na kuielewa mikataba na masharti ya mikopo kabla kuchukua mikopo katika Taasisi hizo .
Taratibu za kushughulikia malalamiko
Kabla ya kuleta malalamiko Benki kuu, mteja atatakiwa kwanza kuwasilisha malalamiko ndani ya taasisi ya kifedha. Ili malalamiko yapokelewe, malalamiko hayo lazima yawe yamewasilishwa Benki Kuu ndani ya muda wa miaka miwili tangu kutokea kwa tukio la kusababisha malalamiko.
Taasisi ya kifedha inapaswa kutatua malalamiko ya mteja ndani ya siku 14 tangu tarehe ya kuleta malalamiko. Ikiwa haiwezi kutatua malalamiko ndani ya muda uliowekwa, itamjulisha mteja mara moja sababu za kushindwa kutatua ndani ya muda pamoja na hatua zinazochukuliwa kwa haraka kutatua malalamiko, na sio zaidi ya siku 7 baadaye.
Endapo mteja akionekana kutokubaliana na uamuzi wa taasisi ya kifedha au akishindwa kupata jibu kutoka taasisi ya kifedha ndani ya siku 14 tangu tarehe ya kuleta malalamiko, anaweza kuleta malalamiko yake Benki kuu ndani ya siku 14.
Aidha BOT imetoa wito kwa Taasisi zote zinazohusisha na biashara kukopesha fedha bila vibali kutoka Benki kuu zihakikishe zihakikishe zinafuata taratibu za kupatia leseni za biashara hiyo kutoka Benki kuu.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.