Wasimamizi wa Vituo vya kupigia Kura pamoja na Makalani wa Vituo vya Kupigia kura Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo wapematiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo kwenda kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 27/11/2024.
Mafunzo hayo yamefanyika Leo tarehe 23/11/2024 katika bwalo la Lwangwa Sekondari.
Akifungua Mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Msimamizi wa Uchaguzi
Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo Adv.Peter Salama amewataka Wasimamizi hao wa Vituo pamoja na Makalani kwenda kutekeleza majukumu yako kwa kuzingatia Sheria kanuni na taratibu na uaminifu ili kufanikisha zoezi la kupiga kura kwa weledi na haki.
Afisa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo Bi.Raheli Ndalusanye akiendesha mafunzo kwa vitendo kwa wasimamizi wa Vituo vya kupigia kura na Makalani wa Vituo katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 27/11/2024.
SIFA ZA KUPIGA KURA
1.Uwe Raia wa Tanzania
2.Uwe na umri wa miaka 18 na kuendelea
3.Uwe Mkazi wa Kitongoji husika
4.Uwe na akili timamu
5.Uwe umejiandikisha katika Orodha ya Wapiga kura
Aidha Vituo vya Kupigia kura vitafunguliwa kuanzia saa 02:00 Asubuhi Hadi saa 10:00 Jioni
"Serikali za Mitaa Sauti ya Wananchi, Jitokeze kushiriki Uchaguzi"
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.