MFUMO WA NeST KATIKA MANUNUZI YA UMMA UTUMIKE KUPUNGUZA HOJA ZA CAG ILI KUAONGEZA UWAJIBIKAJI MKOANI MBEYA .
Watumishi wa Umma Mkoa wa Mbeya, wametakiwa kuutumia vizuri mfumo wa Manununzi ya Umma kwa njia ya Mtandao NeST ili kupunguza hoja CAG katika Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya.
Hayo yameelezwa leo tarehe 27/08/2023 na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Bwana Vincent Agustine Mbua wakati akifunga mafunzo ya siku tano(5)kuhusu Matumizi ya Mfumo wa Manunuzi ya Umma kwa njia ya Mtandao NeST yaliyo wakutanisha watumishi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Bwana Mbua amewasitizia washiriki wa mafunzo hayo kwenda kuwa chachu ya mabadiliko katika kitengo cha manunuzi katika Halmashauri zao kwa kuwafundisha watumishi wengine namna kutumia mfumo wa NeST katika kufanya Manunuzi ili kuongeza ufanisi katika kufanya manunuzi na utangazaji wa tenda kwa wazabuni.
"Yatumieni vizuri mafunzo haya miliyopata ili yakawe chachu ya mafanikio na mabadiliko katika kitengo cha Manunuzi ya Umma kwenye maeneo yenu ya kazi" amesema Bwana Vincent Agustine Mbua
Katika hautua nyingine Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, baada ya mafunzo hayo ametaka Maafisa Masuuli katika Halmashauri zote za Mbeya kuandaa Mpango wa Manunuzi mwaka wa fedha 2023/2024 kupitia Mfumo mpya wa Manunuzi ya Umma NeST hadi kufikia tarehe 05/09/2023.
Kwa upande wao washiriki wa Mafunzo hayo, Wameishukuru Serikali ya Awamu ya sita kwa kuanzisha Mfumo mpya wa Manunuzi ya Umma NeST kwani ni mfumo salama, wenye ufanisi unaokoa muda katika kufanya manunuzi na kutangaza tenda na pia unganishwa na taarifa nyingne muhimu za NIDA na TRA na mifumo yote ya kibiashara.
Mkaguzi wa ndani kutoka Halmashauri ya Busokelo CPA Kabile Mwita amepongeza ujio wa mfumo wa NeST kwani utasaidia Serikali kupunguza hoja za ukaguzi, na kuongeza uwazi na uwajibikaji katika kusimamia ununuzi wa umma.
Maafisa Manunuzi, Wakaguzi wa ndani, Maafisa TEHAMA, Wanasheria, Mafisa Mipango na Maafisa Habari wa Halmshauri saba(7) za Mkoa wa Mbeya wameshiriki mafunzo ya siku5 kuhusu matumizi ya Mfumo wa Manunuzi ya Umma kwa njia Mtandao NeST yalianza tarehe 23/08/2023 hadi leo 27/08/2023 katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.