Mkurugenzi wa Elimu Tanzania kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Bw. Julius Nestory hapo jana amefanya ziara ya kikazi katika halmamashauri ya Wilaya ya Busokelo ili kujionea maendeleo kwa ujumla katika sekta ya Elimu.
Bw. Nestory amepata nafasi ya kutembelea shule ya sekondari ya wasichana ya Busokelo, Shule ya sekondari ya kutwa ya Mzalendo na kisha kufanya kikao cha pamoja cha Wadau na wasimaizi wa elimu katika halmashauri ya busokelo.
Akiongea na wadau na wasimamizi katika ukumbi wa Roman Catholic Lwangwa alipongeza namna kiwango cha elimu katika ufaulu kinavyopanda mwaka hadi mwaka na pia namna ambavyo uongozi unavyosimamia fedha zinazotolewa na Serikali za elimu bila malipo.
“Ninawashuru sana.. ninawapongeza sana kwa namna mnavyokwenda, ndio maana hata Mhe. Rais anapopita anasema kuwa sasa ninwaelewa..”Alisema Bw. Nestory
Pamoja na kujionea changamoto mbalimbali ambazo zinaikaikabili sekta ya elimu katika halmashauri hii amesisitiza juu ya walimu kufanya kazi kwa bidi ili kuleta mapinduzi ya elimu nchini.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.