Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Mhe. Julius Chalya ameagiza maeneo yote yenye vyanzo vya maji yatunzwe na kulindwa kwa kufanya shughuli na kupanda mazao yanayoendana na mazingira hayo.
Akiongea jana wakati wa kuzindua zoezi la upandaji miti katika Halmashauri ya Busokelo, alisema kuwa wananchi wanapaswa kuyalinda maeneo hayo kwa kupanda miti na mazao yanayoendana na mazingira hayo ili kutunza uoto uliopo na upatikakanaji wa maji.
“Kuna maeneo mengi yenye ukame nayo yalikuwa na maji kama yalivyo maeneo yetu. Kila mmoja wetu anapaswa kulisimamia hili ili tusije tukajikuta maeneo yetu yanageuka kuwa jangwa”. Alisema Mhe. Chalya
Wananchi walisema kuwa ipo haja kwa serikali kuweka mkazo na kuwanjengea uwezo wananchi ili waweze kuzalisha miche ya miti ambayo itasaidia kutunza mazingira badala ya kukata miti.
Zoezi la upandaji miti lilihusisha kata za Lwangwa, Kabula,Mpata, Lwangwa na Itete ambapo Halmashauri iligawa zaidi ya miche 167,200 kwa Wananchi ili kwenda kupanda kwenye vyanzo vya maji na maeneo yanayostahili kupanda miti.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.