OBORESHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA UTAHUSISHA UJUZI, WELEDI,UZALENDO NA USHIRIKIANO.
Zoezi la Uboreshaji Daftari la kudumu la Wapiga Kura 2024 linahusisha ujuzi, Weledi, Uzalendo na ushirikiano baina ya Maaafisa Waandikishaji, Wadau wa Siasa na Serikali ili kufanikisha zoezi hilo ufanisi.
Haya yamelezwa leo 16/12/2024 Mkoani Mbeya na Mwenyekiti wa Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe.Jaji Jacobs C.M. Meambegele wakati afungua mafunzo ya siku mbili kwa Maafisa Waandikishaji ngazi ya Jimbo katika Halmashauri za Mkoa wa Mbeya.
Mhe.Jaji Mwambegele amewataka Maafisa Waandikishaji ngazi ya Jimbo katika katika Mkoa wa pamoja na Maafisa TEHAMA kwenda kutumia ujuzi na maarifa watakayopatiwa kupitia mafunzo hayo, kwa weledi, Uzalendo, ushirikiano na kujituma ili kufanikisha zoezi la Uboreshaji Daftari la Kudumu la kupiga kura .
Katika hatua nyingine Mhe.Jaji Mwambegele amesema kuwa Mawakala wa vyama vya siasa Wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya Uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga kura ili kuongeza uwazi na kuwezesha ushirikiano katika kufanikisha zoezi hilo kwani wao ndio wanao watambua Wapiga kura wao katika maeneo husikia
Aidha Mawakala hawataruhusiwa kuingilia majukumu ya Maafisa Waandikishaji katika vituo badala yake watatakiwa kutimiza majukumu yako ya Uwakala kulingana na miongozo na taribu zitakazo tolewa kupitia vya vyao vya siasa.
Zoezi la Uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga kura mwaka 2024 Mkoani Mbeya linatarajia kuanza 27/12/204 hadi tarehe 02/01/2024
Kauli mbiu ya Uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga kura Mwaka 2024 "Kujiandika kwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi
Bora"
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.