Waziri wa Nishati wa Jamhuri ya Muungano, Dkt. Merdad Kalemani ameagiza wakandarasi wanaosambaza umeme vijijini kupitia mradi wa umeme vijijini (REA) awamu ya tatu, kuhakikisha wanasambaza umeme bila kuacha nyumba hata moja.
Hayo yamesemwa jana wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofanyika katika kata ya Lupata, kijiji cha Nsooso katika Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo.
Dkt. Merdad Kalemani amesema kuwa amepata taarifa kuwa wananchi wanapata manyanyaso sana kutoka kwa wakandarasi waliopewa kazi ya kusambaza umeme katika maeneo yao.
“Nyumba hizi tulizonazo ndio za hali zetu, hata kama za ni ya matope au tembe nataka uwake umeme. Kama hakuna jengo lolote kwenye eneo lako na umelipia simika nguzo uwekewe umeme hapo”. Alisema Dkt. Merdad Kalemani
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Wananchi hao walisema kuwa Wakandarasi wamekuwa wakiwaruka katika mgao wa umeme kwa kisingizio kuwa nyumba zao hazina sifa za kuwekewa umeme.
Mradi wa umeme vijijini (REA) umekuwa ukitekelezwa kwa awamu tatu sasa, ambazo awamu ya kwanza ilikuwa ni kufikisha umeme katika vijiji, ikifuatiwa na awamu ya pili ambayo ilihusisha zoezi la kufikisha umeme kwenye vituo na sasa awamu ya tatu inahusisha zoezi la kusambaza umeme nyumba hadi nyumba.
Mradi huu unahusisha vijiji vipatavyo 52 ambavyo vitanufaika kupitia mradi huu katika halmashauri ya Wilaya ya Busokelo.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.