SERIKALI YA AWAMU YA SITA KUTATUA CHANGAMOTO ZA BARABARA KWA WANANCHI WA BUSOKELO.
Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh. Rais Dk.Samia Suluhu Hassan inatarajia kukamilisha ujenzi wa barabara ya Katumba-Mbambo-Tukuyu (km 79.4), Katumba- Lupaso (km 35.3) na Mbaka - Kibanja (km 20.7) kwa kiwango cha lami ili kukuza uchumi wa wananchi wa Busokelo kupitia shuguli za usafirishaji mazao ya kilimo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, Oktoba 1, 2023 katika kijiji cha Kandete, Halmashauri ya Busokelo mkoani Mbeya wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara.
Katika ziara yake, Mh. Bashungwa ameambatana na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, Bashungwa amebainisha kuwa maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuwa Barabara hiyo ijengwe kiwango cha lami ili kuchagiza maendeleo ya kiuchumi kwa jamii ya Busokelo na Mkoa wa Mbeya.
Waziri Bashungwa amebainisha kuwa tayari Serikali imeshatumia kiasi cha fedha Bilioni 21.307 kwa kujenga kwa kiwango cha lami sehemu ya kwanza inayoanzia Bujesi - Mbambo (km 12.7), na Sehemu ya pili inayoanzia Kibanja - Tukuyu (km 7) na mkandarasi kutoka kampuni ya kichina ya China Railway 15 Group kwa muda wa miezi 45.
Aidha, Mh. Bashungwa ameongeza kuwa Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua mchango wa uzalishaji unaofanywa na wana Busokelo na Rungwe kwa ujumla,Mhe Dk. Samia ameelekeza kuwa barabara hiyo ikamilishwe kwa kiwango cha lami katika kipande cha Katumba- Lupaso (km 35.3) na kipande cha Mbaka - Kibanja (km 20.7)
"Mhe. Rais anafahamu barabara hii na ameridhia iwekwe lami na hivi karibuni tunakwemda kutia saini mkataba wa ujenzi na tutamwalika Mhe. Mbunge wa jimbo la Busokelo kuja kushuhudia mkoani Dodoma",amesema Waziri Bashungwa.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.