Serikali imetoa fedha kiasi cha Sh. Milioni 500 kwa ajili ya kujenga kituo cha Afya cha Kata ya Mpata, Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Tangu mwishoni mwa mwaka jana Serikali imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya Ujenzi wa vituo vya afya.
Katika awamu ya kwanza ya utoaji wa fedha hizi, Halmashauri za Wilaya ya Kyela na Rungwe zilinufaika na mpango huu katika Mkoa wa Mbeya. Katika awamu ya pili ya mpango huu umehusisha Halmashauri 161 katika nchi nzima ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo.
Pamoja na kutoa fedha hizo, Serikali imetoa muongozo wa matumizi ya fedha hizo ambapo 15% ya mradi itatekelezwa na jamii kama nguvu kazi na 85% itatekelezwa na Serikali.
Akiwasilisha mradi huo kwa Wananchi wa Kata ya Mpata, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, Bw. Eston Paul Ngilangwa alisema kuwa wanapaswa kujifunza kutoka kwa majirani zetu wa Kyela na Rungwe ambao katika awamu ya kwanza ya mradi huo wamefanya vizuri.
Alisisitiza kuwa mikakati ya utekelezaji wa mradi huu ni pamoja na kuunda kamati ya ujenzi ambayo itahusisha jamii ya Kata ya Mpata pamoja na timu ya Wataalam kutoka Halmashauri. Aidha mradi huu unatakiwa kukamilika ndani ya siku tisini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo akiwasilisha Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya katika Kata ya Mpata
Baadhi ya Wataalam kutoka TAMISEMI na baadhi ya Wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo wakijadili jambo katika eneo linalotarajiwa kujangwa Kituo cha Afya
Diwani wa Kata ya Mpata, Mhe. Mollo akifafanua jambo kwa Wataalam kutoka TAMISEMI na Halmashuri juu ya eneo linalotarajiwa kujengwa Kituo cha Afya.
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wakisikiliza kwa makini juu ya maelekezo ya ujenzi wa Kituo cha Afya katika kata ya Mpata
Timu ya wataalam kutoka Halmashuri wakiwa pamoja na wananchi katika mkutano wa hadhara kujadili na kuweka mikakati ya kutekeleza mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya katika Kata ya Mpata.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.