SHIRIKIANENI NA WATENDAJI WA VIJIJI KUWAHUDUMIA WANANCHI.
Viongozi wa Serikali za Vijiji wametakiwa kufunya kazi kwa weledi, uzalendo na moyo wa kujituma kwa kushirikiana na Watendaji wa vijiji ili kuwatumikia Wananchi kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.
Wito huo umetolewa leo 11/12/2024 na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo Mhe.Anyosisye Njobelo wakatika akifungua Mafunzo ya Uongozi na Utumishi kwa Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na Wajumbe wa Halmashauri za vijiji katika Kata za Mpombo, Kandete, Isange na Luteba.
Zaidi ya Viongozi 400 wa Serikali za Vijiji wakiwemo Wenyeviti wa Vijiji,Wenyeviti wa Vitongoji na Wajumbe wa Halmashaurui za vijiji kutoka ukanda wa Mwakaleli wamepatiwa mafunzo ya Uongozi katika bwalo la Mwakaleli Sekondari ili kuwajengea uwezo wa namna ya kuwatumikia Wananchi katika nafasi mbalimbali za uongozi walizochaguliwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
‘’Baada ya kuchaguliwa na Wananchi wenu, mlikula kiapo cha utii, Mafunzo haya muyatumie vizuri ili mkawatumikie Wananchi katika vijiji venu, kuweni wazalendo, mkashirikiane na Watendaji wa vijiji kutatua kero zote katika maeneo yenu kwa haki, usawa na kujituma ili muwaletee maendeleo Wananchi waliyo wachagua” alisema Mhe.Njobelo.
Kwa Upande wake Afisa Utumishi Halmshauri ya Wilaya ya Busokelo Bw.Fredrick Kweka aliwasilisha mada kuhusu Majumuku ya Wenyeviti wa vijiji, Wenyeviti wa vitongoji na Wajumbe wa Halmashauri za vijiji pamoja na majukumu ya Mtendaji wa kijiji na wajibu wa Serikali za vijiji kwa Wananchi ili kuongeza uelewa katika utekelezaji majukumu kwa viongozi hao.
Katika Hatua nyingine Afisa Mapato Halmashauri ya Busokelo Bi.Abella Ndamugoba aliwajengea zaidi uwezo Viongozi wa Serikali za vijiji kuhusu madhara ya utoroshaji wa mapato na umuhimu wa kusimamia ukusanyaji wa maopato katika vijiji huku akiwataka kutowafumbia macho wale wote wanao shiriki katika utoroshaji mapato kwenye vijiji kwani wanadhoofisha maendeleo ya kijiji husika.
Aidha Bw.Elia Msukwa Afisa Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo aliwaeleza Viongozi hao namna ambavyo migorororo ya ardhi inavyokwamisha shughuli za maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na kijiji kwa ujmla huku akiwataka kutokuwa chanzo cha migogoro ya ardhi na badala yake waishauri jamii kufikia mwafaka mzuri katika utatuzi wa migogoro ya ardhi kwa kuzingatia sheria kanuni na miongozo iliyowekwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, Idara ya Utawala na Rasilimali Watu imeratibu mafunzo ya uongozi na utumishi kwa viongozi wote Serikali za Mitaa waliyongia madarakani mwaka 2024 katika kata zote 13 za Busokelo ili kuwajengea uwezo wa kutwekeleza majukumu yao.
Tayari Viongozi wa vijiji kutoka kataza Isange, Kandete, Luteba,Mpata, Kabula, Lwangwa na Lupata wameshapatiwa mafunzo ya Uongozi , zoezi la utoaji mafunzo hayo linaendelea katika ukanda wa Lufilyo.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.