Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Busokelo, Bw. Eston Paul Ngilangwa ameyaongea haya jana kwenye kongamano la elimu lililofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Lufilyo, Busokelo.
Bw. Ngilangwa amesema kuwa tafsiri iliyopo miongoni mwa jamii kuhusu kauli aliyotoa Mhe. Rais kuhusu chakula mashuleni imetafsiriwa vibaya na wananchi na hivyo kusababisha kurudisha nyuma maendeleo ya taaluma kwa wanafunzi.
“Kuna watu wanafanya jitihada za makusudi kupotosha kauli ya Rais juu ya michango mashuleni, kuna watu wanafanya jitihada za makusudi kuturudisha nyuma. Hatuwezi kuwa na matokeo mazuri kama hatuna mipango thabiti ya kuhakikisha watoto wetu wanapata chakula cha mchana mashuleni”. Alisema Bw. Ngilangwa
Bw. Ngilangwa alisema kuwa yeye kama Mkurugenzi Mtendaji kazi yake ni kusimamia sheria na atahakikisha kuwa anasimamia ajenda ya chakula inakuwa ya kudumu na kama wazazi hawatakuwa tayari basi atawalazimisha.
Wakitoa ujumbe kwenye burudani mbalimbali zilizoandaliwa na wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi na sekondari walisisitiza wazazi wawezeshe upatikananji wa chakula cha mchana mashuleni ili kuboresha maendeleo ya taaluma kwa kupunguza utoro mashuleni.
Kongamano la elimu katika halmashauri ya wilaya ya Busokelo hufanyika kila mwaka kwa kuwashirikisha wadau wote wa elimu. Katika kongamano hili hutolewa zawadi mbalimbali kwa Walimu, Wanafunzi pamoja na shule ambazo zimefanya vizuri na pia zenye changamoto.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.