SUALA LA LISHE NI JUKUMU LA KILA MMOJA, WAZAZI NA WALEZI TUWAJIBIKE.
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe.Jaffar Haniu leo 31/10/2024 amehitimisha Madhimisho ya Siku ya Lishe Kitaifa Katika Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo.
Akiwahutubia Wananchi wa Busokelo katika viwanja vya Lwangwa shule ya msingi, Mhe.Haniu ameeleza kuwa Suala la lishe ni jukumu la kila mmoja hivyo wazazi na walezi wahakikishe watoto wanakuwa na afya bora.
Aidha Mhe.Haniu ameagiza kuundwa kwa klabu za Lishe mashuleni huku akiwasisitiza wazazi wote kuhakikisha Wanachangia chakula cha watoto shuleni ili kuwawezesha watoto kufanya vizuri kitaaluma katika masomo yao.
Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo Bi.Mwanahawa Ntandu akisoma taarifa ya tathmini ya Lishe kwa kipindi cha Julai hadi Septemba 2024, amesema kuwa hali ya udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano ni 2.1%.,hali ya ukondefu ni 1.6%, uzito uliozidi ni 0.4%.
Pia Watoto walizaliwa na uzito pungufu ni2.39% na akina Mama waja wazito waliopatikana na upungufu wa damu ni 0.1%
Katika hatua nyingine,Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe.Haniu amewahimiza Wananchi wote kutimiza haki yao ya Kikatiba kwenda kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 kwa kuchagua Viongozi bora.
‘’Nichukue fursa hii kuwaomba, wale wote tuliojiandikisha katika daftari la wakazi katika uchaguzi wa serikali za mitaa, tumemaliza zoezi hili, nasasa tumebakiwa na zoezi la Uchaguzi, niwaombe wote waliyofikisha umri wa miaka 18 na kuendelea tushiriki uchaguzi kwa kuchagua Viongozi wa Serikali za Mitaa itakapofika Novemba 27 ,2024’’alisema Mhe. Haniu.
Maadhimisho ya Siku ya Lishe katika Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo yamepambwa na michezo mbalimbali ikiwemo, mpira ya miguu,ngoma za asili,buruadani za muziki,na mpira ya net ball.
Kauli mbiu ‘’ Mchongo ni Afya yako, Zingatia unachokula"
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.