Mafunzo haya yametolewa kwa Walimu 41 wa shule za msingi, ambapo program hii inahusisha uundaji wa klabu za TUSEME na kufundisha Stadi za maisha kwa wanafunzi wa shule za msingi. Mafunzo haya yamefanyika kwa siku tatu mfululizo na kumalizika leo, katika katika ukumbi wa kituo cha kilimo kilichopo kandete.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo walimu ili kuitambua vyema program ya TUSEME, kuwezesha uundaji wa klabu na stadi za maisha. Pia kuwezesha walimu kutambua umuhimu wa ufundishaji unaozingatia jinsia (jicho la jinsia) na kuwawezesha walimu kutambua aina za ukatili katika maeneo yao (mashuleni).
Programu hii ya TUSEME inafadhiliwa na shirika la kimataifa linaloshughulika na watoto la UNICEF ambapo kwa sasa inatekekelezwa katika mikoa ya Mbeya, Songwe, Iringa na Njombe.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.