Wadau wa afya wanaondesha ubia katika kutoa huduma za afya jana wamekutana katika mkutano wa robo ya kwanza kujadili utekelezaji na changamoto zinazokabili ubia huo.
Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo kwa kuhusisha wadau mbalimbali wanaoweka ubia na serikali katika huduma za afya ikiwa ni pamoja na taasisi za dini, mashirika yasio ya kiserikali na watu wenye ushawishi kwa jamii.
Katika mkuano huo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji na utoaji wa huduma za afya, mratibu wa ubia ngazi ya Halmashauri Bibi. Laurencia Urio alisema kuwa utoaji wa huduma umeendelea kuimarika siku hadi siku kwa kuongeza idadi ya wataalamu katika vituo vya kutolea huduma.
“huduma zimeendelea kuimarika, kwa mfano katika mwaka 2012 tulikuwa na mganga 1 lakini hadi kufikia mwaka 2018 tuna waganga 8” alisema Bibi. Urio
Bibi. Urio aliongeza kuwa idadi ya wateja imeendelea kuongezeka ikiwa ni matokeo ya kuongezeka kwa idadi ya watu na pia kuimarika kwa huduma katika vituo na hivyo kuvutia watu wengi, wakati idadi ya wanawake wanaojifungua kwenye vituo vya kutolea huduma imeongezeka kutoka 2498 mwaka 2016 hadi kufikia wanawake 2713 mwaka 2018.
Wakichangia mjadala kwenye mkutano huo wadau hao walisema kuwa changamoto kubwa kwenye ubia huu ni uelewa mdogo wa wananchi juu ya ubia wa huduma za afya hivyo kufanya utekelezaji wa baadhi ya majukumu kuwa mgumu.
Mkataba wa utoaji huduma kati ya serikali (halmashauri ya wilaya ya Busokelo) na kanisa la kiinjili la kilutheri tanzania dayosisi ya konde kwa mara ya kwanza ulianza mwaka 2012 ambapo halmashauri ya busokelo ilianzishwa. Katika mwaka huo Serikali iliweza kuingia mkataba na kanisa katika Hospital moja na zahanati 6.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.