WADAU WA VYAMA VYA SIASA BUSOKELO KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA.
Afisa Mwandikishaji Jimbo la Busokelo Wakili.Peter Salama amewataka Wadau vya vyama vya siasa Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo kwenda kuwahamasisha Wananchi wa Busokelo kujitokeza kushiriki zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura kuanzia 27/12/2024 hadi 02/01/2025.
Wakili Salama ametoa wito huo leo 21/12/2024 kwenye ukumbi wa Halmashauri katika kikao maalaumu na Wadau wa Vyama vya siasa, viongozi wa madhehebu ya dini, Wawakilishi wa Wafanyabiashara viongozi wa vyama vya michezo na wawakilishi wa Machifu kutoka Busokelo.
Akifungua Mkutano huo, Wakili Salama amesema kuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi INEC inafanya kazi kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali muhimu wakiwemo viongozi wa dini, viongozi vya vya siasa, Machifu, Wanamichezo na makundi yote ya vijana na Wazee kwa lengo la kuhamasisha jamii ijitokeze kushiriki zoezi la Uboreshi Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
“Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi inatambua mchango wenu, ninyi ni Viongozi mnaoishi na watu hao katika jamii zetu na mnazungumza na Wananchi moja kwa moja kupitia nyumba za ibada, Majukwaa ya siasa michezo , Biashara na shughuli za utamaduni, kila mmoja atumie nafasi yake kuwahamasisha Wananchi kwenda kuboresha taarifa zao pindi uboreshaji utakapoanza’’ Alismea Wakili Peter Salama
Aidha Wakili Salama amesema kuwa Mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kama Waangalizi wa vyama vyao na wao ndiyo wanaowafahamu Wapiga kura wao katika eneo husika na hivyo hawaturuhusiwa kuingilia majukumu ya Maafisa Waandikishaji katika vituo, badala yake watatimiza majukumu yao ya uwakala kwa kuzingatia sheria na miongozo katika kutekeleza zoezi hili.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 17 (1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024, Chama cha Siasa chenye usajili wa kudumu kinaweza kumteua mtu mmoja katika kila kituo cha uandikishaji kuwa Wakala wa Uandikishaji wa Wapiga Kura.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 16 (5) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024, Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utakuwa mara mbili kati ya kipindi kinachoanza mara baada ya uchaguzi mkuu na kabla ya siku ya uteuzi. Wanaohusika katika zoezi hili ni wananchi ambao: -
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.