WALIMU WAMETAKIWA KUWA WABUNIFU KATIKA UFUNDISHAJI ILI KUONGEZA UELEWA KWA WANAFUNZI.
Walimu wametakiwa kubuni njia mbadala za ufundishaji ili kuongeza uelewa kwa wanafunzi na kuwawezesha Wanafunzi mashuleni kunya vizuri katika masomo kuanzia ngazi ya Elimu ya Awali , Msingi na Sekondari.
Hayo yameelezwa leo 01/Juni/2024 na Mwl.Suzana Nussu Mkurugenzi msaidizi aneshughulikia masuala ya Elimu ya Awali na Msingi Ofis ya Rais TAMISEMI katika Kikako kazi cha kuhimiza ufundishaji kwa Walimu wa shule za Msingi na Sekondari kilichofanyika katika shule ya sekondari Lwangwa.
Mwl. Nussu amewaambia Walimu kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuboresha mazingira rafiki ya kufundishia na ujifunzaji pamoja na utatuzi wa changamoto za watumishi wote wa umma ikiwemo Walimu.
‘’Nina salamu zenu kutoka kwa Mhe.Rais Dk.Samia, Mhe.Rais anawashukuru sana kwa kazi nzuri mnayoifanya, hivyo basi Walimu wenzangu ni lazima nina wahimiza tuendelee kufanya kazi kwa umahiri, uweledi na nidhamu ya hali ya juu, vilevile Walimu wa Busokelo naomba nitoe tu ushuhuda, hatuna kesi nyingi za kinidhamu kwa Walimu wa Busokelo, naomba niwapongeze kwa hilo” alisema Mwl.Nussu.
Aidha Mwl.Nussu amesisitiza kuwa msingi mzuri wa ufundisha huanzia katika madarasa ya awali na kuendelea hivyo ni vema Walimu watumie mbinu rafiki na bunifu mbalimbali zinazo endana na mwongozo wa ufundishaji ili watoto waweze kuelewa na kuyashika yale wanayofundishwa darasani .
‘’Walimu wenzangu wajengeeni uwezo mzuri watoto kuanzia madarasa ya Awali ili wawe na umahiri katika masomo yao kupitia kusoma, kuandika na kuhesabu, ikiwemo matumizi ya lugha ya kiingereza’’
Katika hatua nyingine Mwl.Nussu amewataka Walimu wote kudumisha umoja na mshikikamano ili wawze kutumia majukumu yako kwa ushirikiano na hivyo kuleta matokeo chanya kitaaluma na kijamii.
Lwangwa, Tukuyu
Anuani ya Posta: S. L. P. 2, Tukuyu
Simu: +255 737 205 318
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@busokelodc.go.tz
Hakimiliki ©2019 Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo. Haki zote zimehifadhiwa.